Jumapili, 28 Januari 2018

Kilimo cha hydroponic fodder kwa kutumia plastiki ya dumu

UTANGULIZI
HYDROPONIC ni sayansi/sanaa ya
kuotesha mazao bora yenye tija kwa
muda mfupi zaidi bila kutumia
udongo kabisa, kwa kutumia maji na
virutubisho (Hydroponic Nutrients).
HYDROPONIC HYDROPONICS FODDER
– ni kimea kinachooteshwa kwa
kutumia mbegu za shayiri au ngano
ili kupata chakula cha mifugo mfano
kuku, ng’ombe, sungura, nguruwe,
mbuzi, kondoo n.k
Ili kuotesha mbegu zako kwa utaratibu
huu utahitaji kuwa na banda maalum
kwa kuoteshea lenye ukubwa wowote,dumu la rita ishirini la maji Pia utahitaji kuwa na virutubisho vya
hydroponics (Hydroponics Nutrients),
Sprayer (Chupa ya kunyunyiza maji
yenye matundu madogo ili maji
yamwagike kama mvua), Mbegu za
shayiri au ngano (chagua mbegu
ambazo hazijashambuliwa na
wadudu), na pia unatakiwa uwe na
chombo cha kuloweka mbegu na hapa
waweza kutumia ndoo ya aina yoyote,
kwani itatakiwa uziloweke kwa siku
chache.
Sayansi hii ya uoteshaji wa mbegu
mbalimbali madhumuni makubwa
sana ni kwaajili ya mifugo kama vile,
Kuku, Mbuzi, Ng’ombe, kondoo na
kazalika, ila kama ni mboga inaweza
itwa hydrponic tomatoes na kazalika
kulingana na aina ya mbegu husika.
FAIDA YA MATUMIZI YA HYDROPONIC
Ili kuweza kukupatia picha halisi
tunakufahamisha kwanza faida
zilizopo za matumizi ya hydroponic
fodder kwa mifugo.Kwa uchache
baadhi ya faida hizo ni:
• Ni nafuu sana kulinganisha na
garama za CHAKULA cha madukani au
viwandani.
• Kina virutubisho na vitamini mara
3 zaidi ya CHAKULA cha kawaida cha
Mifugo.
• Hupunguza magonjwa ya mfumo
wa hewa kama vile mafua kwa
mfugaji na Mifugo kwani hakina
vumbi kabisa.
• Kina protein na Energy/nishati
nyingi zaidi mara 3 ya inayopatikana
kwenye vyakula vya kawaida vya
Mifugo kama kuku.
• Mifugo hukua haraka sana
kutokana na wingi wa protein ambayo
hufanya Kazi ya kujenga mwili na
kukuza.
• Chakula hiki ni laini sana na
kitamu kwa kuku na mifugo yote
(palatable).
• Mmeng’enyo wa chakula hiki
huongezeka kutoka 30% kwa chakula
cha kawaida hadi 95% kwa chakula
cha hydroponiki hivyo chakula kingi
kutumiwa na mwili wa mifugo na
kupunguza kinyesi na usumbufu wa
usafishaji wa banda.
• Kinyesi hupungua na kuwa kati ya
5%-10% tu kwani chakula kingi
humeng’enywa na kutumiwa na mwili
wa mifugo.
• Mazao kama mayai au maziwa
huongezeka kwa 40% kulinganisha na
chakula cha kawaida.
• Kiini cha yai la kuku anayelishwa
hydroponic fodder huwa cha njano
sana hata kama ni kuku wa kisasa.
• Hupunguza garama za ufugaji
kwenye manunuzi ya chakula kwa
50-75% hivyo kuongeza faida.
Pamoja na mnyumbulisho wa baadhi
za faida ya matumizi ya teknolojia hii
hapo juu,kiujumla ni rahisi kutumia
teknolojia hii kwani inaweza
kufanyika mahali popote. Husaidia
kuvuna na kupata mazao mengi kwa
muda mfupi. Haina madhara kwa
afya za mifugo na binadamu kama
mlimaji alizingatia maelekezo.
JINSI YA KUANDAA
Tumefanya tafiti kufahamu hatua
kadhaa zinazopitiwa ili kufanikisha
zoezi la upandaji.Zifuatazo ni baadhi
ya hatua ambazo tumefanikiwa
kukutana nazo:
• Chukua mbegu zako kisha zisafishe
vizuri kuondoa takataka zote.
• Weka maji kwenye ndoo safi na
kisha weka mbegu zako ili kuziloweka
kwa muda wa masaa 4 au zaidi
ukipenda masaa 12.Muda mrefu zaidi
huwezesha mbegu kuchipua vizuri na
kwa haraka.
• Baada ya masaa 4 au 12 kupita toa
mbegu zako kwenye ndoo na uzichuje
maji kwa kutumia chujio au kitambaa
kisafi.
• Baada ya kuchuja maji hamishia
mbegu zako kwenye dumu ulilolikata katika pande mbili kama inavyoonyesha kwenye picha kisha
zisambaze ili zisibanane kupita kiasi.
Kwa kuanzia fursa hii unaweza
kutumia tray yeyote hata ungo unafaa
kwa kuanzia .

• Baada ya kuweka mbegu zako
funika dumu yako kwa
muda wa masaa 48 (SIKU 2) tumia
mfuniko wenye matundu madogo
madogo na machache.
• Baada ya masaa 48 kupita (siku 2)
mbegu zako zitakuwa zimechipua
kikamilifu, utaona mfano wa nyuzi
nyeupe zinachomozo.
• Hamishia dumu zako kwenye
kichanja au eneo lenye hewa ya
kutosha lakini zikinge dhidi ya jua
kali kwa kuweka turubai au nailoni
juu ya kichanja unaweza pia kutumia
hata mifuko ya unga (viloba)
kutengeneza kichanja, unaweza pia
kuzungusha wavu kama net za mbu ili
kuzuia wadudu i.e inzi na pia kama
eneo lako lina ndege wengi basi
kutumia net itakuwa msaada kwako ili
kuwazuia ndege hao.
UMWAGILIAJI
Mwagilia angalau mara 3 kwa siku,
yaani asubuhi, mchana na jioni.
Hakuna haja ya kumwagilia usiku kwa
sababu hewa ya usiku huwa imepoa
na kubeba unyevu wa kutosha na hata
asubuhi usishangae kukuta umande
kwenye fodder yako.
UVUNAJI
Unaweza kuvuna fodder yako ndani
ya siku 7 au 9.Ingawa wapo wengi
wanavuna haraka yamkini ili kukidhi
uhitaji kwa wakati husika.Lakini
makala nyingi zinaelekeza siku 7 au
9.

Kilimo cha mahindi

UTANGULIZI
Mahindi ni chakula muhimu na ni aina ya nafaka katika mataifa ya Afrika
yaliyomo kusini
mwa jangwa la Sahara. Ni chakula cha matumizi ya nyumbani kwa idadi ya
watu
inayokadiriwa kuwa asilimia 50. Ni chanzo muhimu cha madini na kuongeza
nguvu
mwilini, protini, madini ya chuma (iron) vitamini na madini mengine
asilia.Waafrika
hutumia mahindi kwa njia mbalimbali (uji, ugali na pombe). Na mahindi ya
kuchoma.
Kila sehemu ya mmea wa mahindi ina thamani kiuchumi : punje, majani, shina
na magunzi
huweza kutoa kiasi kikubwa cha bidhaa nyinginezo zilizo chakula na
zisizokuwa chakula.
Vile vile mahindi ni chakula muhimu cha mifugo (ng’ombe) na huhifadiwa kama
silage. Pia
mabaki ya mimea na nafaka na pia hutumika viwandani kutengeneza wanga na
mafuta.
Mahitaji ya mahindi katika hali ya hewa, udongo na Mahindi ni mimea ambayo
hustahimili
mabadiliko mengi ya hali ya hewa na humea katika maeneo mengi tofauti.
Kuna aina nyingi
za mahindi yanayotofautiana katika muda wa kukomaa, mahindi huwa na
ustahimili
mkubwa kwa mabadiliko katika kiwango cha joto. Mahindi haswa huwa mimea
ya maeneo
ya joto ambako unyevu ni wa kutosha.
HALI YA HEWA
Mmea huu unahitaji kiwango cha joto cha kila siku cha nyuzi joto 20º ili umee
vyema. Joto
la juu sana kwa mazao mazuri ni kama nyuzi joto 30º. Hupandwa sana katika
sehemu zilizo
katika kimo cha mita 3000 kutoka bahari hadi kwenye ukanda wa pwani.
mahindi yaweza
kupandwa kama chakula cha mifugo. Hustawi vizuri katika udongo wenye
uchachu wa
soil pH 6-6.5. Na pia Hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko wa
2500m.
Mahindi huwa yanaathirika na ukosefu wa unyevu wakati wa kutoa maua na
matunda. Pia
yanahitaji maji ya kutosha wakati wa kupanda. Katika nchi za joto jingi
(tropiki), mahindi
hufanya vyema katika mvua ya kiwango cha milimita 600 hadi 900 wakati wa
kukua.
Mahindi yanaweza kukuzwa kwenye aina nyingi za udongo lakini hukua vyema
zaidi katika
mchanga, usiotuamisha maji mengi, ulio na hewa ya kutosha na ulio na rutuba
na madini ya
kutosha. Kuwepo kwa mazao mengi ya mahindi kunapelekea kunyonywa sana
kwa madini
kwenye udongo.
Mahindi yako katika kikundi cha mimea kinachoaminika kuathirika na hali ya
chumvi
katika maji na udongo. Kwa vile mimea ambayo ni michanga huwacha sehemu
kubwa bila
kuzingirwa na ardhi, mmomonyko wa udongo na kupoteza maji hutokea sana
sana hivyo
basi ni bora umakini uzingatiwe katika uhifadhi wa udongo na maji kwa kuweka
matandazo (mulching).
KUTAYARISHA SHAMBA
 Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu
uliopita.
 Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
 Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
FAIDA ZA KUANDAA SHAMBA MAPEMA
 Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa
kutumia
jembe lolote.
 Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
 Hupunguza magugu.
 Hupunguza wadudu waharibifu
 Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
 Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au
yatakuwa kidogo.
 Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi na yatastawi vizuri.
WAKATI WA KUPANDA
Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua haitabiriki,Kama mvua hunyesha
nyakati na
majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za
kupanda zao la
mahindi katika eneo lako.
 Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba
mwishoni.
 Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
 Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba
mwishoni
 Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari
mwanzoni.
Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao
mengi ni
mkubwa. Kwa mashamba makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja
kabla ya mvua
kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua. Isiwe mapema zaidi
kwani mbegu
zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu,panya,ndege na wanyama
wengineo.
KUCHAGUA MBEGU BORA
Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
 Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
 Huzaa mazao mengi.
 Hustahimili magonjwa.
AINA ZA MBEGU
 Mbegu aina ya chotara(hybrid)
 Aina ya ndugu moja(synthetic)
 Mbegu aina ya composite
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa
kuzaa magunia
50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja.
MAPENDEKEZO YA MBEGUZA KUPANDA
Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa SIDCO ,PANNAR,
CHOTARA,
kutoka KENYA n.k
KUPANDA
Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani ikizidi
 Kuna uwezekano wa mazao hupungua.
 Mmea huangushwa na upepo
 Mabua mengi hayazai.
 Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababishwa mavuno
kupungua
jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na
mtaalamu
hapo chini.
KIASI CHA KUPANDA
 Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali(sumu)
 Kiasi cha kilo 20(ishirini) za mbegu kinatosha kupanda hekari moja.,
(*Hii hutegemea na aina ya mbegu)
NAFASI ZA KUPANDA.
Hiyo ni baina ya mstari na mstari na mche kwa mche.
 75cm x 30cm mfano:- mstari kwa mstari 75cm na mche kwa mche 30cm
 75cm x 60cm
 90cm x 25cm
 90cm x 50cm
PICHA: Nafasi nzuri ya upandaji
KUTUMIA MBOLEA
 Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwa mbolea pamoja na
matunzo
mengine ya kilimo bora.
 Angalizo: Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.
KUNA AINA MBILI KUU ZA MBOLEA
 Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hua na
virutubisho vya kutosha ambavyo havijulikani vipo kwa kipimo kiasi gani.
 Mbolea za viwandani, hizi hua na virutubisho vya kutosha na vipimo
hujulikana, hii
inasaidia kujua ni kiasi gani kitumike kwa kipindi gani.
KWA MFANO:
Mbolea inayotumiwa na wakulima wadogo mara yingi huwa haitoshi. Mahindi
ya kiwango
cha juu yaweza tu kufikia kiwango cha juu cha Uzalishaji iwapo yatapewa lishe
na madini
ya kutosha. Mahindi ya tani 2 kwa hekta na tani 5 kwa hekta hutumia karibu
kilo 60 N, kilo
10 za P205 na kilo 70 K20 kutoka katika udongo. MAhindi hunyonya Nitrogen
pole pole
katika miezi ya kwanza baada ya kupanda, lakini huongezeka hadi kiwango
cha juu kabisa
wakati wa kutoa maua na kukuza tunda (gunzi). Mahindi huhitaji nitrogen kwa
kiwango
cha juu na ukosefu huwa ndio kizingiti. Kiwango cha juu cha nitrogen
kinahitajika mara
tatu; kwanza wakati wa kupanda, pili, wakati ambapo mmea umefikia sentimita
50 za urefu
na tatu, wakati matunda ya mahindi yanaanza kutoa zile nyuzi nyuzi nyororo
(silking).
Udongo mwingi huwa na madini ya phosphorous (P205) na potassium (K20)
lakini sio
kiwango kinachotosheleza mahitaji haswa ya mbegu za mahindi zinapochipua.
Nyunyuzia
P205 karibu na mbegu ili ziote kwa haraka. K20 hutumika kwa kiwango
kikubwa lakini
hitaji la mimea hubainika baada ya upimaji wa hali ya udongo kujua kiasi cha
mahitaji (soil
test). (ndo maana twasisitiza mbolea za viwandani sio lazima iwe ya
chemical)
DALILI ZA UPUNGUFU WA MBOLEA
Ukosefu wa K20 husababisha ncha za majani kuwa na rangi ya njano na
kuunda gunzi (cob)
lisilo na punje hadi juu. Ukosefu wa P205 hufanya matawi kuwa na rangi ya
samawati na
mbegu zisizo laini. Dalili za ukosefu wa nitrogen ni majani ya rangi ya
manjano na mimea
dhaifu mifupi. Phosphate haifyonzwi haraka na mahindi na pia udongo mwingi
wa nchi za
joto hukosa madini hayo ya phosphate. Inashauriwa unyunyuzie mbolea ya
kiasili kama
samadi kabla ya kulima ili uboreshe hali ya udongo na kuongezea madini.
Katika ukulima wa kiasili, (organic farming), Nitrogen (N) hutiwa kwenye
udongo kupitia
kwa upandaji wa mimea ya jamii ya mikunde (legumes) ambayo hutoa nitrogen
katika
hewa, Hata hivyo mapendekezo ya kimbolea yaliyo katika misingi ya uchunguzi
wa udongo
hutoa nafasi nzuri ya kupata kiasi kizuri cha mbolea bila kuweka kiwango cha
chini au juu.
Omba msaada kutoka kwa mafisa ugani wa kilimo waliyo katika eneo lako.
Katika maeneo
yanayo tegemea mvua kukuza mahindi, panda mbegu wakati wa mvua ya
kwanza. Hii
itaruhusu mizizi kunyonya madini yaliyotengenzwa na bakteria katika udongo.
Maji
yaliyosimama huyeyusha na kuondoa madini ya nitrogen kutoka katika udongo
na
kusababisha ukosefu wa Nitrogen.
KUDHIBITI MAGUGU
Udhibiti wa magugu ni muhimu sana. Katika wiki 4 hadi 6 za mbele baada ya
kumea,
mahindi huathiriwa sana na magugu. Ni lazima mahindi yapandwe mara moja
baada ya
kutayarisha shamba. Unaweza kulima katikati ya laini za mahindi ili udhibiti
magugu.
Nchini Tanzania, kupalilia mara mbili kunahitajika kwa aina nyingi za mahindi,
ingawa
kupalilia kwa mara ya tatu kutahitajika kwa aina ambazo zinahitaji miezi 6
hadi 8
kukomaa. Kupalilia kwa mikono kunahitaji siku 15 kwa hekta la mikono (power
tiller) ni
masaa mawili mpaka matatu kwa ekari.
UHUSIANO WA NIPE NIKUPE
Desmodium (desmodium uncinatum) nyasi ya Molasses (melinis minutifolia)
zikipandwa
kati kati ya laini za mahindi huzuia wadudu kama stalk borers moths. Mimea
hii hutoa
kemikali ambazo huwafukuza wadudu aina stem borers’ moths. Zaidi ya hayo
Desmodium
huzuia gugu haribifu,witchweed striga hermonthica. Napier grass (pennisetum
purpureum) na Sudan grass (sorghum vulgare sodanese) ni mimea mizuri sana
inayonasa wadudu aina ya stem borers.
Napier grass ina njia yake madhubuti ya kujikinga dhidi ya wadudu
wanaotoboa mmea kwa
kutoa utomvu kutoka kwenye shina, ambayo huzuia wadudu kufyoza mmea na
kusababisha uharibifu. Nyasi hizi pia huvutia adui wa stem borers kama
mchwa, earwigs na
buibui. Nyasi aina ya Sudan pia husaidia maadui asilia, kama nyigu (parasitic
wasp).
Mahindi huweka kivuli kwenye mimea ya mboga mboga ikipandwa safu moja
katikati ya
mboga kwenye maeneo yaliyo na jua kali. Hii huongeza mazao ya mboga
zilizopandwa hivi.
na mimea jamii ya mikunde huongeza nitrogen kwenye udongo ambayo
huitajika zaidi
katika ukuaji wa mahindi pia hupunguza wadudu aina ya (leafhoppers,
leafbeatles, stalk
borers na fall army worm), upandaji wa mimea jamii ya mikunde ufanyike mara
baada ya
palizi ya kwanza
UVUNAJI
Uvunaji hufanyika kwa kutumia mikono kwa mashamba madogo na mashine
(combine
harvester) hutumika kwa ajili ya mashamba makubwa, Zao la wastani la
mahindi
ulimwenguni mnamo mwaka 2000 lilikuwa kilogramu 4255 kwa kila hekta. Zao
la wastani
nchini Marekani ilikuwa kilo 8600 kila hekta, huku mataifa yaliyo chini ya
jangwa la Sahara
la Afrika yakivuna kilo 1316 kwa kila hekta ya shamba.
Zao la wastani katika taifa la Tanzania kati ya mwaka 2001-2005 lilikuwa kati
ya gunia
15-19 kwa hekta (sawa na kilo 1350-1750) Ukilima kwa kuzingatia ukulima wa
kisasa na
kanuni zake kwa Tanzania utavuna kilo 5000 kwa hecta (ukanda wa pwani) na
kilo 7500
kwa nyanda za juu kama Iringa, Mbeya, Ruvuma, Arusha n.k
WADUDU NA MAGONJWA YA MAHINDI
WADUDU
1. Vipekecha shina wa mahindi (Busseola fusca; Chilo and Sesamia species)
Vipekecha shina wa mahindi ni wadudu waharibifu wa mahindi, mtama na
mazao mengine
katika nchi nyingi za Afrika. Viwavi wa nondo, huchimba na kuingia ndani ya
shina la
mahindi, wakila tishu za ndani na kusababisha mmea kunyauka na hatimaye
kufa.
Wadudu hao wanaweza kudhibitiwa kwa njia mbalimbali kama mbinu za
kitamaduni, hasa,
kilimo cha mseto na mfumo wa ‘sukuma-vuta’ (‘pushpull’). Pia wanaweza
kudhibitiwa na
dawa za kuua wadudu, unga wa mwarobaini, lakini katika hatua za mapema,
kabla ya
mabuu kuchimba na kuingia ndani ya shina.
2. Osama (Prostephanus truncates)
Dumuzi ‘Osama’ ni mdudu hatari sana wa mahindi ya kuhifadhiwa kote barani
Afrika.
Osama hula ndani ya nafaka na kuacha shimo na ganda tupu. Ghala safi ya
kuhifadhia ni
muhimu ili kuweza kuzuia uharibifu wa osama. Kukoboa nafaka kutoka kwa
gunzi kabla ya
kuhifadhi kunaweza kupunguza uharibifu.
Funza wa vitumba (Helicoverpa armigera)
Funza wa vitumba ni mdudu msumbufu wa mimea mingi muhimu ya chakula,
mafuta na
fedha duniani kote, ikiwa ni pamoja na nafaka mfano Mahindi ikiwa ni
mojawapo, mikunde,
matunda na mboga. Ushambulizi mkali wa viwavi wa nondo huyu kunaweza
kusababisha
hasara kwa mavuno yote.
Kudhibiti kwa njia ya kemikali kunapaswa kufanywa kwa makini na wakati
mwafaka kwa
kuwa viwavi hutoboa na kuingia ndani ya nafaka au matunda ya mmea, hivyo
kuweza
kulindwa. Usugu kwa dawa, kama vile za pyrethroid, kumeripotiwa katika nchi
nyingi.
Bakteria aina ya Bacillus thuringiensis (Bt) na madawa ya mwarobaini hutoa
udhibiti wa
ufanisi dhidi ya viwavi na wakati huo huo kupunguza uharibifu wa maadui wa
kiasili.
Udhibiti muhimu wa kitamaduni ni pamoja na kuondoa na kuharibu mabaki ya
mimea
baada ya kuvuna, kulima udongo ili uwatoe nje pupae na kupanda kwa wakati
mmoja.
MAGONJWA
1. Doa jani la kijivu la mahindi (Cercospora zeae-maydis & Cercospora zeina)
Doa jani la kijivu la mahindi umeibuka kama ugonjwa ulioweka kikwazo kwa
mazao ya
mahindi nchini Marekani na kusini mwa Afrika katika miaka 25 iliyopita. Ingawa
ulidhaniwa kuwa aina moja ya kuvu, Cercospora zeae-maydis, ukaguzi wa
chembechembe
umeonyesha kuwa kuvu lingine, C. zeina, hupatikana kwa wingi mashariki mwa
Marekani
na kusini mwa Afrika. Mbegu za kuvu, zinazoishi katika mabaki ya mazao ya
awali,
hurushwa na matone ya mvua kwenye majani ya chini ya mmea na
kusababisha madoa
marefu yanayoungana kwenye mimea isiyohimili na kusababisha baka. Mashina
hudhoofika na kuanguka wakati wa mikurupuko ya magonjwa.
Ugonjwa unaweza kusimamiwa kwa kuharibu mabaki ya mimea baada ya
kuvuna, kilimo
cha mzunguko, kwa kutumia aina zinazovumilia ugonjwa zaidi, na, matumizi ya
dawa za
kuua kuvu ikiwa zitaleta faida kiuchumi.
2. Muozo wa mahindi na mycotoxin (Fusarium and Aspergillus species)
Kuna aina nyingi za kuvu zinazotokea kwenye mahindi na kuzalisha sumu za
kikemikali
ambazo huchafua chakula na lishe. Zinajulikana kwa pamoja kama mycotoxins,
na sumu
hizi zina madhara makubwa kwa afya ya binadamu na wanyama.
Aspergillus inasemekana kuwa mzalishaji muhimu zaidi wa mycotoxin katika
Afrika,
ingawa kuvu nyingine kama vile Fusarium pia inahusika. Makundi yote mawili
ya kuvu
hukua kwenye sehemu za mimea zilizokufa na zinazooza na kusababisha
kuoza kwa
mahindi katika shamba. Huzalisha unga mwingi wenye mbegu za kuvu juu ya
mahindi,
kabla na baada ya kuvuna, lakini pia inaweza kuwa bila kuzalisha koga lolote.
Muozo wa
mahindi unaosababishwa na kuvu zinazozalisha mycotoxin hutokea kwa wingi
zaidi wakati
mahindi yana matatizo na yanakua vibaya.
Udhibiti bora zaidi wa kuvu hizi huchanganya kuvuna kwa wakati muafaka na
kukausha
mahindi kabla ya kuyahifadhi. Aflasafe™, njia mpya ya kibiolojia ya kudhibiti
Aspergillus,
inatumika katika mashamba kabla ya mahindi kutoa maua na imeonyesha
matumaini
makubwa katika kupunguza uchafuzi wa mahindi kabla ya kuvuna na baadaye
mkusanyiko
wa mycotoxins katika bidhaa zilizohifadhiwa.
3. Ugonjwa wa maize lethal necrosis (Multiple virus infections)
Maize lethal necrosis disease (MLND) ni ugonjwa mpya wa virusi barani Afrika.
Umesababisha wasiwasi mkubwa kwa sababu mimea hufa na hakuna nafaka
au ni nafaka
kidogo tu zinazozaliwa.
Chanzo cha ugonjwa
Wataalamu katika tafiti zao wanasema kuwa, ugonjwa huu husababishwa na
virusi vya aina
mbili vinavyoathiri mmea wa mahindi kwa pamoja ambavyo ni Maize Chlorotic
Mottle
Virus (MCMV) na Sugarcane Mosaic Virus (SCMV).
Virusi hivi husambazwa na wadudu wa aina mbili, ambao ni Thrips pamoja na
Aphids, japo
kuna wadudu wengine wanaweza kubeba na kusambaza ugonjwa huo kama vile
beetles
and leafhoppers pamoja na matumizi ya mbegu zilizoathirika.
 Dalili za mahindi yalioathirika
 Majani machanga ya juu hugeuka na kuwa na rangi ya njano na hatimaye
kukauka
kuanzia pembezoni mwa jani kuelekea katikati na hatimaye mmea kufa.
 Mmea huweza kutoa machipukizi mengi sana.
 Mbelewele hukosa chamvua hivyo mmea kutozaa.
 Mahindi yakishambuliwa wakati yanajaza mbegu, gunzi husinyaa na kuweka
mbegu
chache au kutojaza kabisa.
 Mahindi yaliyoathirika hushambuliwa na magonjwa nyemelezi hasa ukungu.
 Kwa mimea iliyoanza kusinyaa, huonyesha dalili za kukomaa kabla ya wakati,
huku
hindi likiwa katika hali ya kuchoma maganda na kuonesha utayari wa kuvunwa.
Aidha, ugonjwa huo unaposhambulia katika hindi lililokomaa, basi huingia moja
kwa moja katika kiini cha punje.
Mahindi yaliyoathiriwa na ugonjwa huu huota fangas ambayo wataalamu
wanasema
ina sumu kali ijulikanayo kama Aflatoxin. Sumu hiyo, husababisha madhara
kwa
binadamu na wanyama.
Utafiti uliofanywa na wataalamu mbalimbali wakiwepo wataalamu kutoka
Taasisi ya utafiti
wa Kilimo ya Seliani (SARI) wamebaini kuwa, sumu hiyo (Aflatoxin)
inayotokana na
fangasi, husababisha ugonjwa wa saratani ya ini kwa binadamu na wanyama.
Utafiti huo
pia unaeleza kuwa, ugonjwa huo unaweza usionekane kwa haraka na huweza
hata
kuchukua muda wa mwaka ndipo kujitokeza.
Hivyo basi, ni lazima mataifa yote kuwa makini na kuchukulia jambo hili kwa
uzito zaidi.
Mbinu za kuepuka ugonjwa huu
• Panda mbegu bora zilizothibitishwa na Taasisi ya Uthibiti wa Ubora wa
Mbegu (TOSCI)
nchini.
• Usipande mbegu zilizovunwa msimu uliopita kutoka katika shamba
lililoshambuliwa na
ugonjwa.
• Safisha shamba kwa kuondoa magugu na masalia yote ya mazao na
kuyachoma/kuyafukia kuepuka maficho ya wadudu na virusi vya ugonjwa.
Kagua shamba
mara kwa mara na kama utaona dalili zilizotajwa hapo juu, toa taarifa kwa
mtaalamu wa
kilimo aliye karibu nawe.
Namna ya kudhibiti
• Ng’oa mapema mahindi yote yaliyoathirika, na kuyateketeza haraka.
• Usipande mahindi katika shamba lililoathirika angalau kwa msimu mmoja.
Panda mazao
mengine kama vile viazi mviringo, mihogo kama utakavyoshauriwa na
mtaalamu wa
kilimo.
• Katika maeneo yenye ugonjwa, dhibiti wadudu wasambazao ugonjwa huo kwa
kunyunyizia kiuatilifu kulingana na maelekezo ya mtaalamu.
• Zingatia kilimo cha mzunguko wa mazao na toa taarifa mapema kwa afisa
ugani wa kilimo
endapo utaona dalili za ugonjwa.
Ugonjwa wa MLND bado unafanyiwa utafiti kwa undani zaidi na dawa bado
haijapatikana.
Hivyo wakulima wote wanatakiwa pindi wanapoona kuna dalili zozote
zimeanza kujitokeza
katika mashamba yao, hawana budi kung’oa mimea yote bila kujali kama
mengine
hayajaambukizwa kasha waziteketeze kwa moto. Hii ni kutokana na sababu
kuwa hata
mimea ambayo bado haijaonesha dalili za kuambukizwa, hana budi kuonesha
dalili
mapema kwani maambukizi husambaa kwa kasi sana na kwa muda mfupi.
4. Ugonjwa wa matupa kwenye mahindi (SMUT).
Ugonjwa huu hushambulia sehemu za uzazi za mahindi. Mashambulizi
hufanywa na aina
mbili za vimelea jamii ya uyoga (ukungu) vijulikanavyo kwa majina ya
kitaalamu
kama Sphacelotheca reliana na Ustilago maydis. Vimelea hivyo husababisha
magonjwa ya
aina mbili ambayo dalili zake zinafanana. Mimea iliyoshambuliwa na ugonjwa
huu ama
haizai kabisa ama inazaa kiasi kidogo ukilinganisha na jinsi ambavyo ingeweza
kuzaa kama
isingekuwa imeshambuliwa. Kwa hiyo mashambulizi ya magonjwa haya
husababisha
hasara ya mavuno.
Inakadiriwa kwamba hasara ya mavuno inawezakuwa kidogo tu ama asilimia
kumi (10%)
au hata zaidi ya kiwango hicho, lakini kupoteza ni kupoteza hata kama ni
kiwango kidogo.
Ugonjwa wa "matupa" unaosababishwa na kimelea kijulikanacho kama Ustilago
maydis hufahamika kama "Common Smut" kwa kiingereza.
Dalili zake huwa kuota kwa uvimbe katika sehemu za mmea zinazokua kama
vile punje za
mahindi, mbelewele na hata kwenye majani. Uvimbe huo ukikauka na kupasuka
hutoa
vumbi jeusi kama masizi ambayo ndiyo viini vya/mbegu ya huo ugonjwa. Dalili
ya msingi
ya ugonjwa huu kwenye mhindi ni kwamba inawezekana kuwa na baadhi ya
punje
zilizoshambuliwa na zingine ambazo hazina dalili katika gunzi moja.
Ugonjwa wa "smut" unaosababishwa na kimelea kijulikanacho kwa jina
Sphacelotheca
reliana hufahamika kama "Head smut" kwa kiingereza. Kama ilivyo kwa
ugonjwa wa
"smut" ya kawaida, dalili za ugonjwa huu hujitokeza mara nyingi katika hindi
lenyewe na
mbelewele na mara chache katika shina la mhindi. Tofauti na ugonjwa wa
"smut" ya
kawaida, katika ugonjwa huu badala ya mhindi kuathiriwa baadhi ya punje,
hindi zima
hujaa vumbi jeusi ndani ambapo kwa nje ni kama mfuko mweupe ambao kabla
ya kukauka
hufana na uyoga. Vumbi hilo jeusi ndilo viini vya kimelea. Vivyo hivyo kwenye
mbelewele.
Wakati mwingine mmea ulioshambuliwa na ugonjwa huu hudumaa na
hushindwa kuzaa.
Dalili nyingine ya ugonjwa huu ni mhindi kuotesha vijani vidogo badala ya
mbelewele.
UDHIBITI WA MAGONJWA YA"SMUT"
1. Tumia mbegu bora ingawa mpaka sasa haipo mbegu maalumu yenye
kustahimili
ugonjwa huu. Kwa kutumia mbegu bora, mkulima utajihakikishia mavuno bora.
2. Daima hakikisha unalima kilimo cha kisasa kikijumuisha urutubishaji wa
udongo.
Epuka kuijeruhi mimea uwapo shambani. Mimea iliyo na majeraha
hushambuliwa kwa
urahisi na ugonjwa huu. Pia dhibiti wadudu waharibifu ambao pamoja na
madhara mengine wanayosababisha pia huijeruhi mimea na kwa hivyo
kurahisisha
maambukizo ya ugonjwa huu wa "smut".
3. Kila inapowezekana tumia kilimo cha kubadilisha mazao. Katika kubadilisha
mazao ni
vema kutumia mzunguko wa mazao yasiyoshambuliwa na ugonjwa wa "smut"
kama vile
ngano, shayiri, njegere, viazi na maharagwe.
4. Unapolima hakikisha masalia mabua yamefukiwa chini sana.

Kilimo cha pilipili mbuzi

KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI
KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI : Pilipili mbuzi ni zao ambalo
linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao
hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua angalau kiasi cha masaa 6
kwa siku.
Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili,
undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.
Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa pH ni chini
ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya
udongo imefika 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna
ya kuipunguza.
Kuandaa miche.
Mbegu za pilipili huoteshwa miche kwenye kitalu kabla ya kwenda
kupandikizwa shambani. Pandikiza mbegu kwenye kitalu week 7 hadi
10 kabla ya kipindi ambacho umepanga kupandikiza miche
shambani. Panda mbegu tatu tatu kwenye kila kishimo na chagua
mbili zilizo chipua vizuri kwa ajili ya kuhamishia shambani.
Kuhamishia miche shambani.
Hamisha miche shambani ikiwa imetengeneza majani 8, ingawa
kuhamisha ikiwa na majani machache au mengi zaidi haitapelekea
shida yoyote.
MUHIMU… Unashauriwa kuhamisha miche shambani kwa kuzingatia
mambo yafuatayo.
Siku ya kwanza kwa lisaa limoja weka miche kivulini au mahali
ambapo kuna kizuizi jua la moja kwa moja lisiifikie miche. Kadri
siku zinavyo kwenda ruhusu miche kupata mwanga wa jua zaidi.
Chimba mashimo marefu kuzidi urefu wa mizizi ya miche kisha
changanya vyema udongo na mbolea ya Ngo’ombe. Muda mzuri
wa kuhamisha miche yako shambani ni jioni au kipindi ambacho
jua limefifia kuepuka miche kukauka.
Changanya sulphur (Tembe 2) kwenye maji na kumwagilia na
rudia mchanganyo huu kila baada ya week mbili. Sulphur husaidia
kuuwa fungus, inauwa bacteria wasio faa, kuzuia magonjwa pia
huasaidi mizizi kusambaa na kukua kwa haraka na kupata
virutubisho.
Mwagilia miche maji ya kutosha baada ya kuihamishia shambani
hiyo husaidia kupunguza stress za mmea unapobadilishiwa
mazingira. Tumia mbolea ya Miracle Gro kila baada ya week mbili.
Mahitaji ya mmea.
Pilipili ni zao lenye kuhitaji zaidi unyevu unyevu shambani ila maji
yasiwe yenye ktuama. Kipindi ambacho maua yametoka na vitunda
vya pilipili vimeanza kujitokeza, udongo ukiwa mkavu sana hauna
unyevu wa kutosha hupelekea maua kudondoka. Epuka umwagiliaji
ulio zidi mahitaji au ulio chini ya mahitaji. Unaweza kutandaza nyasi
kwaajili ya kusaidia kuhifadhi unyevu shambani. Mmea huanza kutoa
maua mapema baada ya kutengeneza matawi, Maua ya mmea hua
na set iliyo kamilika (jike na dume) hivyo kuwa na sifa ya kuweza
kujichavusha yenyewe.
Upepo, wadudu au kwakutumia mkono husaidia kuongeza
uchavushaji.
MBOLEA
Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia mbolea,wakati huu
tumia Yaramila winner 5-10g kwa mche.NB:Usitupie juu..hakikisha
mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na
mmea,weka 4-6 cm kutoka kwenye mmea.
Na kila baada ya siku 21 weka mbolea aina ya Yaramila winner au
NPK Isipokuwa wakati maua yameanza weka Yaramila nitrabo au
CAN 10g /plant,na baada ya hapo utaendelea na Y-winner mpaka
mwisho wa mavuno.
KUPALILIA
Pilipili zi zao ambalo halina mizizi merefu sana, hivyo basi mkulima
anapaswa kuzingatia hilo na kuongeza umakini wakati wa kupalilia
kuepuka kukata mizizi.
MAGONJWA
1. Fusarium wilt (Mnyauko)
Njinsi ya kuepuka. .Tandika shamba lako na majani makavu ili
kupunguza joto.
Ng’oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki.
Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba
na chini ya miguu uingiapo shambani.
Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya
kutosha.
Pulizia dawa ya fangas kama vile ortiva.
2) Southern blight ( Sclerotium wilt)
Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi
weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected
plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea
muda mfupi kipindi cha joto kali.
Kuepuka/Kuzuia.
Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi waende
chini sana ambapo mizizi haifiki.
Mimea iliyoshambuliwa…Ing’oe yote na choma moto lakini chomea
nje ya eneo la shamba.
Pulizia Ortiva.
3) Anthracnose.
Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa
huweza kukaa ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama
kuna sehemu zinakuwa nyeusi na panajaa majimaji …dalili hii huenea
sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.
Kuepuka.
Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu..Baada ya kuvuna
choma mabaki yote.
Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo
zaidi ya mara mbili…badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio
jamii moja na pilipili mbuzi (Do crop rotation).
Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu…kwa hiyo mkulima lazima
achukue mbegu kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na
mwaminifu…mbegu hazitakiwi kutengenezwa kutoka kwenye
mimea iliyoathirika na ugonjwa.
4) Bacteria.
Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda….huweza kutokea na
kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia
huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.
Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na
pia kwenye matunda.
Kuepuka.
Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu
ugonjwa.Nunua kutoka kwa wakala.
Pulizia dawa yoyote copper.
5) Virusi.
Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili mbuzi.
Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .
Kuepuka.
Nunua mbegu bora
Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na
kuendelea.Wadudu wanaosababisha virus sanasana na wadudu
mafuta (Aphids) kwa hiyo akikisha muda wote shambani hakuna
hao wadudu kwa kupulizia Actara.
NB:Pamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila
kupiga dawa ya wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna
ugonjwa.
Wadudu.
Pilipili mbuzi hushambuliwa na ;
1. Wadudu mafuta ( Aphids)
Kuwadhibiti.
Tumia Actara 8g/20L.
Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.
2. Crickets
Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka
walipo jificha na kukata miche michanga.
Kawadhibiti.
Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na kuwaacha
katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama
ni miche na iko kwenye tray…basi weka hizo tray juu ya kichanja.
3. Beetle.
Tuma Karate 40cm/20L.
4. Utitiri
Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.
5. Nematodes
Tumia solvigo.
Mavuno.
Pilipili huwa tayari kwa kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemea na aina
ya mbegu uliyotumia. Chuma kwa uangalifu bila kung’oa mmea ili
uendelee kuzalisha. Muvuno yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi
1 hadi 3.
Usalama wakati wa uvunaji.
Pilipili huwa na kemikali iitwayo capsaicinoids ambayo inaweza
kukuwasha kwenye ngozi au kwenye macho ikiwa utajigusa. Vaa
gloves wakati wa kuvuna na kuwa mwangalifu usijiguse kwenye
macho.
SOKO
Fursa
Pilipili ni zao ambalo halina mbadala wake au (substitute) hivyo
kufanya mahitaji yake kuwa ni ya muda wote bila kutetereka.
Changamoto
Muda ambao wakulima wengi wanakuwa wamezizalisha zaidi
huathiri sana soko la pilipili kwa maana hata bei ikishushwa sana
haiwezi kushawishi watumiaji kutumia pilipili nyingi zaidi.
Kuepuka changamoto hiyo wakulima wanashauriwa kupunguza
huduma shambani hadi pale soko litakapo tengemaa vizuri.
Mbinu za mafanikio kwenye kilimo hiki.
1. ZALISHA KWA WINGI
Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo
haziepukiki yani (Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama
ndogo utaweza pia uza bidhaa zako kwa bei ndogo na bado utapata
faida nzuri na kujihakikishia soko la uhakika kwa bidhaa zako.
2. TAFUTA MASOKO YA BIDHAA KABLA YA KUANZA UZALISHAJI
Mkulima mwenye mafanikio ni lazima pia awe mfanya biashara mzuri
ukiachilia mbali kuwa mzalishaji mzuri. Mkulima ni vyema
kutengeneza channels mapema kupata wateja wa mazao yako.
Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo itakusaidia sana kwenye
kupata masoko utakwa na ushawishi zaidi kwa wateja. Tengeneza
wateja na wateja watakutengenezea biashara.
Mteja anataka vitu vitatu vya msingi.
Unafuu wa bei
Ubora wa zao
Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa
Ukijihakikishia hivyo vitu vitatu hapo juu hapana shaka utakuwa
umejihakikishia soko la uhakika.
3. USILIME KWA KUFUATA MSIMU
Unapolima kwa kufuata msimu, mtajikuta wakulima wengi
mmezalisha zao fulani kwa wiiingi kwa kipindi kimoja hivyo kupelekea
upatikanaji wa zao hilo kuwa mkubwa kuliko inavyo hitajika kwenye
masoko, jambo hili hupelekea mazao kuuzwa kwa bei ndogo na
kupelekea wakulima kukosa faida ya kutosha au hata kupata hasara
muda mwingine.
Unapolima kwa kutofata msimu mkulima utaweza kuazalisha zao/
mazao kipindi ambacho wengine hawazalishi hivyo mahitaji
yatakuwa makubwa na upatikanaji wa zao hilo utakuwa ni mdogo
hivyo mkulima ataweza kupanga bei nzuri kwa mazao yake.
4. USIFANYE KILIMO KWA MAZOEA
Tumia wataalamu wa kilimo
Tumia njia za kisasa za kilimo
Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka kufanya (Tumia
wataalamu)
Fanya kilimo cha umwagiliaji uweze kuzalisha kipindi ambacho
wengine hawawezi kuzalisha ili uuze mazao yako kwa bei nzuri
zaidi,
FAIDA ZA KUTUMIA PILIPILI
1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu.
2. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene
(overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa
mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti
iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi
Julai 2006.
3. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili
kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha
insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.
4. Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na
vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata
nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu
moja ya mwili.
5. Pilipili husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba
kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi.
6. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye
tumbo (Stomach Cancer).
7. Pilipili husaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo
husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua
kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.
8. Kula pilipili husaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi
cha fibrin katika damu

Kilimo cha nyanya

JUtangulizi:
• Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa
ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa
kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini.
Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na
baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.

Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania
Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na
Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama; Malawi,
Zambia na Botswana.
Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya,
uganda na Tanzania.
Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji
wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga
yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni
jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya
mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo
yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi
na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto),
Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida. Morogoro ndiyo inayoongoza kwa
kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari
15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye
maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana.
Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi,
upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za
nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu,
wadudu, magonjwa na magugu.
Mazingira
• Hali ya Hewa:
Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani
kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko
wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.)
• Udongo:
Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa
kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe
na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na
uchachu wa wastani yaani pH 6.0 – 7.0.
Aina za Nyanya
Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi
mawili:
1. Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina
hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji
wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6,
yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx,
Roma VF (nyanya mshumaa)
Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili:
1. OPV (Open Pollinated Variety) – Aina za kawaida
2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo
zipo aina fupi na ndefu.
Katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na
wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na
zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku
nyingi bila kuharibika mapema.
Kwenye Kilimo – 2
Kuandaa Kitalu cha Nyanya
Mambo muhimu ya kuzingatia:
• Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
• Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
• Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo
ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana
nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
• Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi
mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
• Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa
urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu
nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu
nyingine.
Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya
Aina ya matuta:
– matuta ya makingo (sunken seed bed)
– matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
– matuta ya kawaida (flat seed beds)
Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta
• Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili
mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila
kukanyaga miche].
• Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili
mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
• Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8
ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
• Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au
mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.
• Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua
moja) mraba.
• Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza
kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili
kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa
chini mno kiasi ambacho hazitaota.
Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu
1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds);
– matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye
udongo kwa urahisi zaidi.
– Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi
– Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi
kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara.
Hasara:
o Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo
kama hayakutengenezwa vizuri.
2. Matuta ya makingo (sunken seed beds):
Faida:
· matuta haya ni rahisi kutengeneza
· hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
· nyevu mdogo unaopatikana ardhini
· ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
· huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
· huzuia mmomonyoka wa ardhi
Hasara:
· Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye
· mvua nyingi.
3. Matuta ya kawaida (flat seed beds):
Faida:
· ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
· na kusambazwa mbegu huoteshwa
· ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu
Hasara:
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua
nyingi.
Kusia Mbegu
• Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni
(germination test)
• Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini
mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
• Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
• Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni
vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
• Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha
usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na
mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.
Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini
zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza
msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile
kinyausi (damping off) au ukungu (blight).
• Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa
mbegu.
• Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha
kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini
Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo
Kitaluni
• Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu
nyevu uliopo kwenye udongo.
• Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili
kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga.
(kipindi cha baridi si muhimu sana)
• Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo
miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 – 4. Hii itapunguza
magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na
yenye nguvu.
• Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia
shambani.
• Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya
kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.
Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani
(Transplanting
Rules)
• Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche
shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na
udongo.
• Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa
katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
• Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza
kusababishwa na jua.
• Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari
kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na
mizizi mingi iliyostawi vizuri.
• Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche
yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa
kupeleka shambani.
• Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa
kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
• Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa
toka kitaluni.
• Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili
kutoharibu miche/mizizi.
Maandalizi ya Shamba la Nyanya
• Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
• Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu
yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
• Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia
sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
• Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x
(50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha
baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu
mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi.
Jinsi ya kupanda miche:
• Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
• Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
• Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa
bustanini.
• Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye
udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu
unaosababishwa na mionzi ya jua.
Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani
• Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo
yaliyoko shambani mapema
• Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha
magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
• Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu
zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
• Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha
kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo
na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya,
hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea
unyevunyevu.
Asante sana:
Kwa leo tutaishia hapa, kwenye makala zifuatazo tutajikita kuchambua
baadhi ya wadudu wasumbufu kwa nyanya, tutaangalia pia masoko ya
nyanya pamoja na teknolojia mbalimbali za uzalishaji pamoja na
usindikaji.

Kilimo cha korosho

UTANGULIZI
koroshoo ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae 16
century ndipo lilipo fika africa katika nchi ya mozamboque na baadae
likafika Kenya na Tanzania.
kwa hapa Tanzania korosho ulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya
kusini Mtwara, lindi, na maeneo kama Mafia, bagamoyo na Rufiji.
mvua; korosho ustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm - 1250
mm wastani wa mvua kwa mwaka,
napia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa wa bahari.
udongo; korosho ukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa
kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi kichanga.
KUANDAA SHAMBA
kama mazao mengine shamba la korosho linatakiwa kusafishwa,
kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho.
nakatika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe
ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba.
KUPANDA
Ni muhimu sana kuchagua mbegu bora kwa kua mbegu utakayo panda
ndo itakuonesha kiasi gani utavuna,
baada ya kununua mbegu unachukua maji na chumvi 100g
ya chumvi unaweka katika maji kiasi cha lita 5 unakoroga
vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo
zile zitakazo zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa
kiota,
baada ya hapo unazianika vizuri hili ziweze kukauka
napia unashauriwa kuto panda mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja,
nafasi ya kupanda 12m x 6m kwenye maeneo mvua na kiasi cha miti
kitakua 139/hectare
kwenye maeneo yasio na mvua za kutosha ni 12m x 12m na kiasi cha miti
ni 69/ hectare
MUHIMU
Kuna aina mbili ya kupanda mbegu ya korosho
kupanda moja kwa moja; hii ni njia mambayo ni risk sana
na inaitaji umakini kwa sababu kunauweze3kano mkubwa wa
mbegu kufa. ukitumia njia hii unatakiwa kupanda mbegu tatu
3 katika shimo moja na baada ya miezi mi 3 - 4 ngoa mimea
na bakiza mmoja wenye afya na muonekano mzuri.
njia ya kitaru; hii ni njia ya pili na ni nzuri kwa sababu
unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na
muonnekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani
ikiwa na umri wa wiki 6 na zingatia kuchagua mche wenye
afya.
na baadae unatakiwa kupunguza majani urefu wa sm60- 90 kutoka
kwenye ardhi na pia ondoa majani yote ambayo yanaonekana kuadhiliwa
na magonjwa au wadudu na yale yalio kauka.
MAGONJWA NA WADUDU
MAGONJWA
Anthracnose
powdery mildew
hayo ni magonjwa yanayo athiri thana korosho
WADUDU
Cashew stem girdler
cashew weevil
coconut bug
heliotropes bug
meal bug
trips aphids
KUZUIA NA TIBA
ili kuzuia maagonjwa na wadudu unatakiwa
palilia mapema
weka shamba katika hali ya usafi
tumia mbinu ya kuchanganya mazao kwa korosho unaweza
kuchanya pamba au maharage hiyo inasaidia kukimbiza
wadudu wengine ambao wanakua hawapatani na mazao hayo
tumia pesticide kutibu magonjwa
tumia insecticide kuuwa wadudu waalibifu.
KUVUNA
Korosho ufikia hatua ya kuzaa matunda pale inapo kua na umri wa miaka
2 1/2 hadi miaka mitatu
napia matunda ukomaa pale inapo kua na miaka 9 hadi 10
uwezekano wa mkoroso kuishi ni miaka 30 hadi 40
na kuvuna hua kunaanza mwezi october hadi mwezi december
MATUMIZI
chakula
hutumika kutengeneza rangi
kama zao la biashara
miti yake hutumkia kama kuni
kutengeneza dawa e.t.c

Jumapili, 21 Januari 2018

SULUHISHO KWA MKULIMA WA MAHINDI

AUXO ni kiuagugu chenye wigo mpana wa kudhibiti magugu nyasi na yale yenye wigo mpana kwenye mahindi baada ya magugu na zao kuota
kiuagugu hiki kina viambata amilifu vifuatavyo
1.tembotrione
2.bromoxynil
3.isoxadifen

jinsi kiuagugu kinavyofanya kazi
1.tembotrione hufanya kazi kwa kuingilia mfumo wa vimengenya vinavyosababisha mimea kutengeneza ukijani ambavyo vinaharibiwa na kuruhusu mwanga mkubwa kupenya ndani ya majani na kuyababua

2.bromoxynil inafanya kazi kwa mguso kwa kuingilia usanisi nuru ambapo mfumo wa ukuaji wa mmea hudhurika na mwishowe hufa

3.isoxadifen iliyosajiliwa na bayer pekee ni kinga salama inayozuia mahindi yasidhulike

dawa hii inadhibiti magugu yote ya kawaida na kudumaza ndago kwenye zao la mahindi hasa kama ikitumiwa kwa vipimo vilivyopendekezwa wakati magugu ni machanga na yanakuwa kwa upesi

kwa matokeo bora
1.tumia maji lita 80 adi 120 kwa ekari ili kulowanisha magugu vizuri
2.piga dawa wakati upepo umetulia ili kuepusha dawa kupepelushwa
3.usipige dawa kama mvua inatarajia kunyesha ndani ya masaa ma wili
4.piga dawa wakati magugu ni machanga

FAIDA ZA AUXO
. inaua magugu ya majani mapana na nyasi
. inadhibiti ndago
. uthibiti wa magugu bila kuleta madhara kwa zao

je unaijua dawa ya THUNDER suluhisho kwa wakulima wa mahindi ambao wanasumbuliwa na wadudu wafuatao katika mazao yao
. minyoo wa ardhini
. viwavijeshi
. bungua
. kimamba
. vithiripi

THUNDER ni kiatilifu chenye wigo mpana wa kudhibiti wadudu wanaofonza na kung'ata.
. ufanisi wa kufanya kazi ina muunganiko wa nyia ya mpenyo na mguso na kumuadhiri mdudu kwenye ulaji.
. inafanya kazi haraka na inadumu kwa muda mrefu

kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba za simu
0758583098/0787794298
au whatsapp no 0758583098

KILIMO CHA NYANYA

KILIMO BORA CHA NYANYA
MAGONJWA NA WADUDU
Utangulizi
Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote
(masika na kiangazi), na faida hupatikana haraka na ni ya kuridhisha ikilinganishwa
na mazao mengine. Pamoja na umuhimu wa zao hili, wadudu waharibifu na
magonjwa huathiri uzalishaji na ubora wa matunda. Ili mkulima aweze kupata faida
na kuongeza pato la kaya yake ni vema kuzingatia udhibiti wa magonjwa na wadudu
wa zao hili. Kipeperushi hiki kinatoa maelezo ya udhibiti wa magonjwa na wadudu
muhimu ya zao la Nyanya.
MAGONJWA YA NYANYA
Bakajani chelewa (Late blight)
Ugonjwa huu huenenzwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na hali ya hewa hasa
ya unyevunyevu, na huenezwa na upepo. Majani, shina, matunda hushambuliwa.
Majani huwa na ukungu mweupe na kijivu, na baadaye hukauka. Matunda huwa na
mabaka ya kikahawia na baadaye kuoza. Mashina pia huwa na mabaka ya kikahawia.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa ya kuzuia ukungu hasa wakati wa masika, Dawa
zinazopendekezwa ni Ridomil, Dithane 45, Bravo, Funguran, milraz.
• Fanya mzunguko wa mazao. Usipande nyanya sehemu moja kila msimu au
palipolimwa mazao jamii ya nyanya km viazi mviringo, bilinganya, aina zote
za pilipili na nyanya chungu.
• Tumia mbegu safi
• Panda aina za nyanya zinazovumilia ugomjwa
Bakajani tangulia (Early blight)
Huenezwa na vimelea vya fangasi. Husababishwa na kuenezwa na hali ya hewa
pamoja na mbegu zenye ugonjwa. Mabaka ya kahawia yenye mistari ya mviringo
huonekana kwenye majani na shina. Baka jeusi hutokea sehemu ya tunda
inayoshikana na kikonyo.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa ya Kocide, Funguran
• Teketeza mabaka ya mazao baada ya kuvuna
• Tumia mbegu safi na bora
Mnyauko fusari (Fusarium wilt)
Huenezwa na mbegu zenye ugonjwa. Husambazwa na vimelea vya fungasi
vinavyoishi kwenye udongo.
Ugonjwa hujitokeza zaidi wakati wa kiangazi. Vimelea hushambulia sehemu au
mirija ya mmea ya kupitishia maji na chakula. Mmea hukosa maji na chakula na
hatimaye hunyauka. Shina la mmea likipasuliwa ndani huonekana rangi ya kikahawia.
Udhibiti
• Tumia mbegu safi na bora
• Tumia mzunguko wa mazao. Nyanya zisizungushwe na mazao jamii yake
• Teketeza masalia ya mimea
• Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko bacteria (Bacterial wilt)
Ugonjwa husababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye udongo.
Huenezwa na kusambazwa na mbegu na udongo wenye vimelea. Mirija ya mimea ya
kupitishia maji na chakula hushambulia na mimea hunyauka ghafla. Mmea hukauka
na kufa.
Udhibiti
• Panda mbegu safi
• Panda nyanya sehemu ambayo haijawahi kupandwa viazi mviringo,
bilinganya au nyanya chungu
• Tumia mzunguko wa mazao
• Hakikisha mfereji wa maji ya kumwagilia hayapiti kwenye shamba lenye
historia ya ugonjwa huu.
• Choma kitalu cha nyanya kabla ya kusia mbegu
Mnyauko vetisili (Verticillum wilt)
Hakuna dawa inayozuia au kutibu ugonjwa huu kwa sasa. Ugonjwa husababishwa na
ukungu (fangasi) kwenye udongo. Ukungu huu huishi kwenye udongo kwa muda
mrefu bila kudhurika. Ugonjwa huongezeka ikiwa mizimizi ya nyanya
imeshambuliwa na minyo fundo; au kukiwepo na hali ya ubaridi au ukame. Ugonjwa
husababisha hasara kubwa. Ugonjwa hushambulia sehemu ya ndani ya shina na
kusababisha sehemu hiyo kuwa na rangi ya kijivu. Majani hugeuka njano na mimea
kunyauka na kufa.
Udhibiti
• Tumia mzunguko wa mazao usiopungua miaka mine
• Ondoa mabaki ya nyanya shambani
• Tumia mbegu bora na safi
Bakadoa (Bacterial spot)
Ugonjwa huu huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu, pia
kwenye hewa. Huenezwa kwa kasi sana wakati wa masika. Madoa ya rangi kahawia
huonekana kwenye majani na matunda.
Udhibiti
• Panda mbegu bora na safi
• Tumia mzunguko wa mazao
• Teketeza masalia ya mazao
• Nyunyizia dawa ya funguran, Kocide101, Cobox, Bravo
Makovu bakteria (Bacterial canker)
Ugonjwa huenezwa na vimelea vya bacteria vinavyoishi kwenye mbegu na hewani.
Hutokea zaidi wakati wa masika. Majani hukauka nchani na makovu yaliyodidimia
hutokea kwenye shina. Matunda huwa na makovu yenye rangi ya kahawia sehemu ya
katikati.
Udhibiti
• Tumia mbegu bora na safi
• Teketeza masalia ya mazao
• Tumia mzunguko wa mazao

Rasta (Yellow leaf curl)
Ugonjwa huu husababishwa na virusi na huenezwa na nzi wadogo weupe. Hutokea
zaidi wakati wa kiangazi. Mimea hudumaa na majani yaliyoshambuliwa huwa na
rangi ya manjano na pengine rangi ya zambarau. Nyanya hupasuka.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa za sumu za kuua wadudu (Selecron, Dursburn, Actelic)
• Ng’oa mimea yenye ugonjwa
• Tumia mzunguko wa mazao
• Weka shamba katika hali ya usafi
Batobato (Tomato mosaic virus)
Ugonjwa husababishwa na virusi na hueezwa na mbegu na kugusana. Majani huwa na
mchanganyiko wa rangi hasa kijani kibichi na kijani kilichofifia (majano). Majani
hujikunja na manjani machanga huwa na maumbile yasiyo kawaida. Ukifikisha jani
huwa linavinjikavunjika.
Udhibiti
• Tumia mbegu bora na safi
• Ng’oa mimea iliyoshambuliwa
• Teketeza masalia ya mazao
• Weka shamba katika hali ya usafi
WADUDU WAHARIBIFU
Viwavi Matunda (Fruit worm)
Viwavi hawa hutokana na wadudu nondo. Viwavi hutoboa matunda na kuacha
matundu na hatimaye matunda huoza. Hupunguza ubora wa matunda.
Udhibiti
Nyunyizia dawa ya kuua wadudu. Dawa hizo ni pamoja na Actelic 50EC, Selectron,
Dursbaan, Maji ya majani ya mwarobaini au utupa pia huua wadudu.
Utitiri wekundu (Red Spider mites)
Hawa ni wadudu wekundu, wadogo sana wanaoweka utando chini ya majani, hasa
wakati wa kiangazi. Wadudu hawa hufyonza utomvu kwenye majani na kusababisha
majani kukauka.
Udhibiti
• Nyunyizia dawa za sumu. Dawa hizo ni pamoja na Actellic, Selecron,
Dursbarn na Thionex
• Mwagilia maji mara kwa mara
• Weka shamba katika hali ya usafi
Inzi weupe (White flies)
Hawa ni Inzi weupe wadogo sana. Hujitokeza sana wakati wa kiangazi. Hueneza
ugonjwa wa virusi ujulikanao kama Rasta.

Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Selecron, Actellic, Dursban na
thionex. Pia maji ya majani ya mwarobaini na utupa.
Vidukari au Wadudu mafuta (Aphids)
Ni wadudu wenye rangi nyeusi au kuijani au kahawia. Hukaa chini ya majani na
kufyonza utomvu kwenye majani machanga. Hudumaza mmea na kushindwa kuzaa
matunda
Udhibiti
Nyunyizia dawa za sumu za kuulia wadudu kama Rogor, Actellic, Selecron, Dursban
maji ya majani ya mwarobaini na utupa, maji ya pilipili.
Minyoo (Nematodes)
Ni minyoo midogomidogo ambayo hushambulia mizizi na kuweka vifundo. Mizizi
hushindwa kuchukua maji na chakula kwenye udongo. Mimea hudumaa na
kushindwa kuzaa
Udhibiti
• Tumia mzunguko wa mazao
• Choma udongo wa kitalu kabla ya kusia mbegu kwa kutumia karatasi la
plastiki jeusi na nishati ya jua
• Choma masalia ya mazao
Sota (Cutworms)
Hushambulia miche ya nyanya hasa baada ya kupandikizwa shambani. Wakati wa
mchana hujificha kwenye udongo na usiku hujitokeza na kukata miche kwenye shina
usawa wa udongo.
Udhibiti
• Nyunyiza dawa za kuua wadudu kwenye shina usawa wa udongo
• Hakikisha miche inapata maji ya kutosha.

JIFUNZE KUSINDIKA NYANYA

                              KUSINDIKA NYANYA
Nyanya ni zao ambalo haliwezi kuifadhika kwa muda mrefu lisipozindikwa zao hili ni zao la bustani ambalo linalimwa na wakulima na linahitajika katika shughuli za jikoni kama kiungo cha kuungi  mboga, wakulima wemgi wamekuwa wakipata hasara kwa kulima zao la nyanya na kukata tamaa ya kulima zao hili tena ni kwanini kwa sababu bei ya zao hushuka pale ambapo zao hilo linapatikana kwa wingi sokoni na kumfanya mkulima ashidwe kupata faida kwa sababu zao linapokuwa lipo kwa wingi sokoni na uhitaji wa watu ni mdogo bei hushuka lakini kunakipindi ambacho zao halipatikani kwa wingi sokoni na kuwa na bei kubwa kipindi hiki ni kipindi ambacho mkulima ambaye ni mbunifu anatengeneza pesa lakini atatengenezaje pesa ni kwa kuchakata zao hilo na kulihifadhi na kuuzwa kwa bei ya juu.
Zao la nyanya ni zao ambalo hisindikwa na kupata bidhaa mbalimbali kuepuka uhalibifu wa zao hilo, kuongeza ubora na thamani, na kuwezesha upatikanaji wakati wote, zao hili huzidhikwa kuwa nyanya za kukausha,juice,lahamu na sosi au rojo.

KUKAUSHA NYANYA
Nyanya zinazotakiwa ni zile zilizokomaa na kuiva vizuri. Aina ya nyanya zinazotakiwa ni zile zenye nyama nyingi kama roma, Tanya na tengeru 97.

Vifaa
Visu vikali visivyoshika kutu
Ungo
Sufuria
Jiko
Kaushio bora
Mifuko ya plastiki
Beseni
Jinsi ya kukausha
chagua nyanya zilizokomaa na kuiva vizuri
osha kwa maji safi na salama
kata nyanya kwenye vipande visivyozidi muilimita tano
panga kwenye kaushio safi ili zikauke
fungasha vipande vya nyanya vilivyokauka kwenye mifuko safi ya plastiki isiyopitisha unyevu
weaka lebo inayoonyesha muda wa kuisha matumizi kwa mwaka mmoja kutoka siku  ya kutengenezwa
hifadhi sehemu yenye ubaridi na kavu.
Hutumika kama viungo kwenye vyakula mbalimbali

KUSINDIKA NYANYA KUPATA JUISI
chukua nyanya zilizoiva na kukomaa vizuri
osha kwa maji safi na salama
katakata nyanya katika vipande vidogo
pima uzito wa nyanya
kwa kilomoja ya nyanya ongeza maji lita moja
chemsha kwemye moto kwa muda wa dakika 5 moto uwe na nyuzi joto 85
saga nyanya kwa kutumia mashine ya mkono au umeme
chuja rojo ili kupata juisi
ongeza sukari gram 20 na chumvi gram 10 kwa kila lita moja ya rojo
chemsha tena kwa muda wa dakika 20
jaza juisi ikiwa ya moto kwenye chupa safi
zipange chupa hizo kwenye sufuria
weka maji kwenye sufuria yafii nusu ya chupa
chemsha tena ili kuondoa hewa iliyoupo ndani ya chuapa
ipua acha zipoe kisha weka lebo
ifadhi kwenye ubaridi
juisi hii huifadhiwa kwa muda wa miezi sita
hutumika kama kiburudisho

Jumamosi, 20 Januari 2018

Mbolea ya asili isiyo na kemikali

MBOLEA YA ASILI
MBOLEA VUNDE
1. Namna ya kutayarisha Mboji/Mbolea Vunde/
Mbolea Hai
Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya
mimea na wanyama (matamahuruku))
ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu
ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo.
Sehemu za vitu kama majani, matunda
na mabaki ya mboga hutengeneza
mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa
huku ni tofauti kabisa na zile sehemu
zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika
rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu
na hunukia vizuri.
Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama
zake ni za chini sana na inafaa mno
kuongezwa kwenye udongo ili kuinua
mazao ya shamba.
Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe
mara nyingi huwa vimejazwa
nyumbani au shambani bila mpangilio
wowote. Hivi vinaweza kutumika
kutengenezea mboji lakini itachukua
muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo
rotuba yake kupotea. Lakini kama muda
ukitengwa ili kushugulikia mbolea
matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa.
Mabaki kutoka shambani na jikoni
yanatumika katika kutengenezea mboji.
Mboji iliyotunzwa vyema huwa na
rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa
shambani. Mboji huchemka hata kiasi
cha kuua magonjwa ya mimea na
mbegu za magugu.
Majani makavu ya ndizi ni mazuri kwa
kutunza vifaa vya mbolea na kuweka
ukavu. Hali hii huwa huzuia kupotea
kwa maji kabla ya kujenga lundo la
mboji na wakati mbolea inapokuwa
inaiva.
1.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji
  Sehemu za mimea ambazo
zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua
wadudu (viuatilifu) na kwekwe juzijuzi
(Pesticide/herbicides).  Vipande vya
nyama kwa sababu vinavutia panya na
wadudu wengine. Sehemu nyingi za
Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya
mimea na wanyama (matamahuruku))
ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu
ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo.
Sehemu za vitu kama majani, matunda
na mabaki ya mboga hutengeneza
mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa
huku ni tofauti kabisa na zile sehemu
zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika
rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu
na hunukia vizuri. Maelezo ya msingi
kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea ,
Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama
zake ni za chini sana na inafaa mno
kuongezwa kwenye udongo ili kuinua
mazao ya shamba. Vipande vya vitu au
sehemu ya viumbe mara nyingi huwa
vimejazwa nyumbani au shambani bila
mpangilio wowote. Hivi vinaweza
kutumika kutengenezea mboji lakini
itachukua muda mrefu kabla ya kuoza,
na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini
kama muda ukitengwa ili kushugulikia
mbolea matokeo yatakuwa mazuri na
ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na
jikoni yanatumika katika kutengenezea
mboji.  Mboji iliyotunzwa vyema huwa
na rutuba nzuri kwa mimea
inapotumiwa shambani. Mboji
huchemka hata kiasi mimea na majani
ambazo ziliambukizwa ugonjwa.  Vifaa
vilivyo na ncha kali kama mwiba
ambavyo vyaweza kujeruhi mikono na
miguu. Magugu ambayo yanarudiarudia
kila mwaka. Magugu kama hayo
huuliwa kwa kuanikwa kwenye jua kali
ili yakauke baadaye huchomwa ili
yasienee na jivu lake huongezwa kwenye
biwi, matunda na mabaki ya mboga hutengeneza
mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa huku ni
tofauti kabisa na zile sehemu zilizowekwa. Mboji
iliyoiva hubadilika rangi na kuwa ya hudhurungi,
tifutifu na hunukia vizuri.
Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama
zake ni za chini sana na inafaa mno
kuongezwa kwenye udongo ili kuinua
mazao ya shamba.
Vipande vya vitu au sehemu ya viumbe
mara nyingi huwa vimejazwa
nyumbani au shambani bila mpangilio
wowote. Hivi vinaweza kutumika
kutengenezea mboji lakini itachukua
muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo
rotuba yake kupotea. Lakini kama muda
ukitengwa ili kushugulikia mbolea
matokeo yatakuwa mazuri na ya kufaa.
Mabaki kutoka shambani na jikoni
yanatumika katika kutengenezea mboji.
Mboji iliyotunzwa vyema huwa na
rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa
shambani. Mboji huchemka hata kiasi
cha kuua magonjwa ya mimea na
mbegu za magugu.
Majani makavu ya ndizi ni mazuri kwa
kutunza vifaa vya mbolea na kuweka
ukavu. Hali hii huwa huzuia kupotea
kwa maji kabla ya kujenga lundo la
mboji na wakati mbolea inapokuwa
inaiva.
1.1 Vifaa visivyofaa kuwekwa kwenye mboji
  Sehemu za mimea ambazo
zimenyunyiziwa dawa ya kuwaua
wadudu (viuatilifu) na kwekwe juzijuzi
(Pesticide/herbicides).  Vipande vya
nyama kwa sababu vinavutia panya na
wadudu wengine. Sehemu nyingi za
Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya
mimea na wanyama (matamahuruku))
ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu
ili kusazwa na viumbe vidogo vidogo.
Sehemu za vitu kama majani, matunda
na mabaki ya mboga hutengeneza
mbolea ya mboji. Matokeo ya kusazwa
huku ni tofauti kabisa na zile sehemu
zilizowekwa. Mboji iliyoiva hubadilika
rangi na kuwa ya hudhurungi, tifutifu
na hunukia vizuri. Maelezo ya msingi
kuhusu mboji/mbolea vunde/mbolea ,
Mboji ni rahisi kutengeneza, gharama
zake ni za chini sana na inafaa mno
kuongezwa kwenye udongo ili kuinua
mazao ya shamba. Vipande vya vitu au
sehemu ya viumbe mara nyingi huwa
vimejazwa nyumbani au shambani bila
mpangilio wowote. Hivi vinaweza
kutumika kutengenezea mboji lakini
itachukua muda mrefu kabla ya kuoza,
na hivyo rotuba yake kupotea. Lakini
kama muda ukitengwa ili kushugulikia
mbolea matokeo yatakuwa mazuri na
ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na
jikoni yanatumika katika kutengenezea
mboji.  Mboji iliyotunzwa vyema huwa
na rutuba nzuri kwa mimea
inapotumiwa shambani. Mboji
huchemka hata kiasi mimea na majani
ambazo ziliambukizwa ugonjwa.  Vifaa
vilivyo na ncha kali kama mwiba
ambavyo vyaweza kujeruhi mikono na
miguu.huwa vimejaa nyumbani au
shambani bila mpangilio wowote. Hivi vinaweza
kutumika kutengenezea mboji lakini itachukua
muda mrefu kabla ya kuoza, na hivyo rotuba
yake kupotea. Lakini kama muda ukitengwa ili
kushugulikia mbolea matokeo yatakuwa mazuri
na ya kufaa. Mabaki kutoka shambani na jikoni
yanatumika katika kutengenezea mboji.
 Mboji iliyotunzwa vyema huwa na
rutuba nzuri kwa mimea inapotumiwa
shambani. Mboji huchemka hata kiasi
mimea na majani ambazo
ziliambukizwa ugonjwa.
 Vifaa vilivyo na ncha kali kama
mwiba ambavyo vyaweza kujeruhi
mikono na miguu.
 Magugu ambayo yanarudiarudia kila
mwaka. Magugu kama hayo huuliwa
kwa kuanikwa kwenye jua kali ili
yakauke baadaye huchomwa ili
yasienee na jivu lake laweza kuongezwa
kwenye lundo la mbolea.
 Vitu visivyo kua na uhai kama plastiki
na chuma.
1.2 Mfano wa vitu vinavyoweza kutumiwa
kutengenezea mboji nyumbani
2. Namna ya kutengeneza mboji ya mimea
Kusanya vitu na vifaa vinavyohitajika
katika utengenezaji wa mboji ambayo
ni;
 Majani mengi mabichi/kijani na
makavu. Majani jamii ya mikunde ni
mazuri sana kwani hutengeneza
kirutubishi cha naitrojeni (N) kwa
wingi.
 Mabua ya mahindi au vitawi vya miti
 Udongo wa kawaida wa juu
 Samadi, mbolea yoyote ya wanyama
au mboji ya zamani
 Majivu au vumbi la mkaa
 Maji
2.1 Hatua
1) Chagua sehemu karibu na eneo
ambalo mboji itaenda kutumika na
ambapo kuna hifadhi ya kutosha
kukinga dhidi ya upepo, jua na mvua.
2) Katakata majani yawe madogo
madogo ili yaweze kuoza haraka.
Tengeneza msingi kama mita sita (6)
urefu na upana wake mita 2 kwa
kutumia majani magumu kama matawi/
vijiti. Hii itahakikisha maji yanatiririka
na hewa ina zunguka vizuri. Hakikisha
kuna nafasi ya kutosha kufanyia kazi
kwenye biwi bila kulikanyaga.
3) Weka sentimita 10 ya majani ambayo
hayaozi haraka kwa mfano mabua vya
mahindi au mimea mibichi/kijani.
4) Weka sentimita 10 ya vifaa ambavyo
huoza haraka kwa mfano maganda ya
mboga na matunda.
5) Weka sentimita 2 ya samadi (mbolea-
hai ya wanyama), mabaki ya mbolea ya
zamani kama yaweza kupatikana.
6) Weka udongo wa juu sentimita 10
kutoka kwenye shamba ambalo
hulimwa.
7) Majivu na mkojo vyaweza
kunyunyuziwa juu ili kufanya biwi/
lundo kuoza haraka. Kukatakata majani
8) Nyunyizia maji kwenye biwi mpaka
lilowe.
9) Rudia mpangilio huu kuanzia namba
nne (4) mpaka lundo lifike mita moja
(1.m) hadi moja na nusu (1.5m) kwenda
juu isipokuwa vijiti/matawi ya kwanza.
2.2 Zingatia
 Biwi/lundo cha mboji kinatakiwa
kifunukwe ili kupunguza/kuzuia mvuke
ama mvua nyingi ambayo hubeba
rotuba kutoka kwenye mbolea. Weka
gunia, nyasi ama matawi ya ndizi
yaliyokauka.
 Kila tabaka/kunjo/safu yafaa
kupangwa kuanzia kwenye ukingo ili
lundo la mbolea lisiporomoke.
 Namna nyigine ya kuzuia lundo
kuporomoka ni kwa kuweka vipande
vya mbao kando ya biwi. Wavu wa
nyuzi za chuma utafanya biwi kukauka.
3. Wadudu wenye manufaa na mazingira
yanayohitajika kwenye Biwi
3.1 Wadudu ambao husaidia kufanya biwi kuoza
Viumbe wengi wanaohusika na kazi hii
ya kuoza ni wadogo hawaonekani kwa
macho matupu. Ila viumbe hawa
huhitaji maji, hewa na vipande/sehemu
ya viumbe wengine ambazo kwao ni
chakula. Viumbe hawa hula vipande
hivyo na hutoa hewa ya carbon dioxide ,
maji na joto.
Kuna hatua tatu kubwa wakati biwi
linapooza; hatua ya kupanda joto, hatua
ya kupoa/kuwa baridi na hatua ya
kukomaa.
Wakati ya hatua ya kupanda joto , joto
hufikia kiwango cha juu sana katikati
mwa biwi. Uzuri wa joto hili ni
kwamba magonjwa yaliyokuwa kwenye
viungo vya biwi na mbegu za magugu
huchomwa hadi kufa. Hatua ya pili ya
kuwa baridi; uyoga (fungi) huwa na
faida nyingi kwa sababu kazi yake ni
kuzisaga nyuzi ngumu ambazo zimo
kwenye viungo vya mimea au majani.
Kwenye hatua ya tatu, ‘ hatua ya
kukomaa’ viumbe wakubwa kama
mchwa na nyungunyungu husaidia
kusaga na kuchanganya mbolea.
Hali ya anga ikiwa na joto jingi viumbe
hawa hufanya kazi haraka kuliko
wakati ambapo hali ya anga ni baridi.
Aina ya viungo vilivyotumika kujenga/
kukuza biwi na ukali/uchungu (pH) wa
udongo pia huathiri kiwango cha
mbolea kuoza.
3.2 Mazingira yanayohitajika kwenye biwi
Biwi huhitaji vitu vitatu: hewa, maji na
joto.
Hewa
Viumbe wadogo kwenye biwi huhitaji
hewa ili waweze kuishi. Hewa ya
carbon dioxide (CO2) ambayo imetolewa
na wadudu hawa huhitaji kutolewa nje.
Ikiwa hewa safi itakosekana, viumbe
wengine wasiohitajika huingia na kutoa
harufu mbaya na pia kufanya mbolea
isioze haraka.
Maji
Kazi ya viumbe wadogo huwa polepole
ikiwa biwi ni kavu. Aidha ikiwa biwi
litalowa maji basi viumbe wadogo
watakufa na kufanya biwi kuwa na
uchachu badala ya kutengeneza mbolea.
Hivyo basi kukagua kiwango halisi cha
maji huhitaji ujuzi fulani.
Joto
Biwi hutoa joto wakati linaoza. Lundo
likiwa na joto jingi viumbe wadogo
hutoka, kisha huweza kurudi pindi
linapopoa.
4. Matunzo ya Biwi
Ili kupata mbolea nzuri, biwi
linapojengwa yafaa lishughulikiwe kwa
utaratibu. Biwi hilo litahitaji maji,
kupinduliwa, joto na muda unaofaa wa
kukomaa.
4.1 Maji
Wakati wa kiangazi biwi/lundo la mboji
huhitaji kumwagiliwa maji kila wiki.
Maji katika lundo la mbolea hupimwa
kwa kuweka fungu dogo la nyasi na
kulitoa baada ya dakika tano. Nyasi
isipoonyesha majimaji au unyevu
itabidi maji yamwagwe kwenye lundo
hilo.
Kuna njia kadha za kuzuia mvuke
kuinuka kutoka kwenye biwi, hali
kadhalika kiwango cha maji
yanayomwagiliwa:
 Funika lundo kwa majani ya ndizi
ama nyasi.
 Funika lundo kwa udongo.
 Lundo lisigeuzwegeuzwe
Biwi likilowa maji itabidi kifunuliwe na
kuachwa kikauke kwenye jua kabla ya
kujengwa tena.
4.2 Kupindua/kugeuza
Katika muda wa wiki tatu (3) baada ya
kujenga/kukuza biwi/lundo ukubwa
wake utakuwa umepungua sana.
Kupindua biwi uhakikishe ya kwamba
majani yaliyo kando yameoza pia hewa
safi imerejeshwa. Kupindua biwi
huchanganya majani yaliyotengenezwa
na kukijenga upya. Majani yalivyo
kando huwekwa katikati, ikiwa kuna
ukavu, maji mengi na majani/viungo
vikavu huongezwa. Kupindua
kunatikiwa kufanyike kila baada ya
wiki tatu.
Hali ya joto na kiwango cha maji yafaa
kupimwa siku chache baada ya
kupinduliwa. Kupinduliwa kwa mara ya
tatu kutahitajika ikiwa viungo
havitakuwa vimeoza kikamilifu.
Mbolea yaweza kutengenezwa bila kupinduliwa
ila viungo vilivyo kando havitaoza. Mbegu za
magugu na viungo na magonjwa ya mimea
hayatakufa. Viungo vilivyobaki hutengwa na
kutumiwa kwenye biwi lingine. Japokuwa
kugeuza hakuna lazima, kunapendekezwa ili
kupata mbolea nzuri.
4.3 Kiwango cha Joto
Kupima kiwango cha joto kwenye biwi kunahitaji
kijiti kirefu kichomwe ndani ya lundo siku kumi
(10) baada ya kujengwa. Kijiti yafaa kionyeshe
joto la kutosha kinapoguswa kwa mkono, la
sivyo kuoza bado hakujaanza kufanyika. Katika
hali kama hii, maji ama hewa itahitajika kwenye
biwi na biwi kuachwa kwa muda. Ikiwa biwi lina
joto jingi, biwi linaoza basi viumbe hai wanaweza
kufa. Katika hali hii, hewa na maji itabidi
kuongezwa ili kufanya biwi lipoe. Kiasi cha joto
yafaa kupimwa mara kwa mara kwa kutumia
kijiti.
Chini ya 57C
Joto hili linaweza kuivisha mboji lakini
haliwezi kuua mbegu za magugu na
magonjwa.
57-71C
Joto muafaka kwaajili ya kuivisha mbojj
na kuua mbegu za magugu na
magonjwa. Katika kiwango hiki cha
joto, mbegu zote na vijimelea vyote vya
magonjwa vilivyoko kwenye
mchanganyiko wa mboji hufa na hivyo
kutokuwepo pale mboji inapokuwa
imeiva.
Zaidi ya 71C
Joto hili ni kali sana na huweza
kusababisha madhara mengineyo kama
vile kuzalishwa kwa gesi zenye madhara
pia wadudu wenye manufaa ambao
husaidia mboji kuiva huweza
kukimbia.
Muhimu kuhakikishakuwa joto halizidi
sana ili kuweza kuwa na mboji bora
yenye virutubisho

Ijumaa, 19 Januari 2018

MAGONJWA YA MIHOGO

MAGONJWA YANAYOSUMBUA ZAO LA MUHOGO SHAMBANI

Zao la mhogo halina magonjwa mengi lakini ugonjwa wa "Cassava
Mosaic" na Batobato ndiyo yanayoathiri sana uzalishaji wa zao hili.Ugonjwa huu
husababishwa na virusi na huenezwa na nziwadogo weupe.Mmea ulioathirika
ukitumika kwa vipando mche mpya nao utakuwa na ugonjwa huu.Majani ya mmea
ulioshambuliwa yatakuwa na rangi ya njano na yasiyo na umbo la kawaida.
Kuzuia ugonjwa huu-panda aina ya muhogo inayostahimili ugonjwa
huu,Panda vipandikizi ambavyo havijatoka katika mmea ulioathirika na ugonjwa
huu,pia unaweza kuchovya mbegu ulizokata katika maji ya moto kwa muda mfupi na
kwa tahadhari kubwa.Pia tumia dawa za wadudu kuua nzi weupe.
Kuna magonjwa mawili ambayo yanasababisha kupunguza uzalishaji wa
zao la muhogo shambani.

(A)UGONJWA WA MATEKENYA/ MICHIRIZI YA KAHAWA KATIKA

MUHOGO.
Huu ni ugonjwa ambao unapatika katika sehemu za miinuko iliyo na
urefu chini ya mita 300 na unapatika katika sehemu ndgo katika maeneo ya miinuko
ya mita 500.Ugonjwa huu unaenezwa na mdudu mweupe au inzi mweupe (whitefly)
mwenye mabawa madogo.
Dalili za ugonjwa kwenye mmea wa muhogo.
Hapa tutaangalia katika sehemu tatu za mmea wa muhogo

(I)KATIKA MAJANI
Dalili ya kwanza:hutokea rangi ya njano pembezoni mwa vena ndogo
baadae huathiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa la rangi ya njano.
Dalili ya pili:rangi ya njano ambayo haihisishwi vizuri na vena
isipokuwa katika mabaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za
ugonjwa sehemu kubwa lamin inaweza isiathirike,majani yenye ugonjwa hubaki
yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.

(II)KWENYE SHINA
Ugonjwa huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani lakini jeraha
la zambarau au kahawia linawweza kuonekana nje na kuingia ndani hadi kwenye
gamba baada ya kubandua gome la nje.

(III)KWENYE MIZIZI
Kifo cha mzizi hutokea kuanzia miezi mitano toka kupandwa,dalili za
mizizi huonekana kubadili nje ya mizizi na zinaweza kuwa kama kizuizi mwanga au
shimo au kufa kwenye gome.Tishu inayozunguka mashina ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi,wakati mwingine mizizi huonenekana kuwa yenye afya kwa nje
bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa,lakini ikikatwa
huonekana kufa.Ugonjwa huu uenezwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye
mimema iliyoathiriwa.

(B)UGONJWA WA BATOBATO/UKOMA WA MAJANI
Ugonjwa huu ulienea Tanzania kataka miaka ya 1894 na kuripotiwa
katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.Ugonjwa huu usababishwa na inzi mweupe
lakini uchunguzi wa mara kwa mara umetambua kuwepo kwa virusi vya aina
mbalimbali kama vile; Afrika cassava mosaic virus na Indian cassava masaic virus.

Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
-Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.Piakloritiki ya
jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe yenye
kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.
Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri
sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za awali za
ukuaji wa jani.

Pia majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja
na kujitenga kwa sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
Ugonjwa huu huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa
kawaida hutumika kuzalishia mmea.

JINSI YA KUDHIBITI MAGONJWA HAYA SHAMBANI MWAKA
-Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya
mihogo unatakiwa kuchoma moto ili kutokomeza ugonjwa huo
-Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa
kung’oa ile Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
-Pia unahitajika kuelewa dalili za magonjwa kwa ajili ya kuchukua
tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.

Jumatatu, 8 Januari 2018

ufugaji wa sungura

UFUGAJI BORA WA SUNGURA
UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu
MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki
UFUGAJI WA NJE
1 - Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3 - Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng'oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, usiweke vya plastiki maana huvitafuna na kuwaathiri au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku
CHAKULA
Wapewe majani makavu kwani muhimu sana kwa ajili ya mfumo wa kumeng'enya chakula, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates) Kiasi cha protini wanachohitaji ni 17%
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto
MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake zinahitaji kupunguzwa zikikua sana waone maofisa ugani wa mifugo wakusaidie kwa hili
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba na pia weka mkono mmoja kwa chini ili kusapoti uzito
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo

UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA

JIFUNZE KUFUGA KIBIASHARA HASA KWA WAFUGAJI WA KUKU KWA YOYOTE ATAKAYE HITAJI TEMPLATE HII NA ZINGINE ANITAFUTE KWENYE NO 0756841313