MAAJABU YA MKOJO WA SUNGURA
Licha ya kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kwaajili ya nyama, zao la Mkojo wa Sungura kwa faida yake pengine ndo kubwa kuliko mazao mengine yote
MATUMIZI YA MKOJO WA SUNGURA
Kutokana na kuwa na kiwango kik cha madinitrogen phosphorus na potassium mbolea ya Mkojo wa Sungura imekua mbadala wa mbolea za NPK na CAN ambazo kwa kiasi kikubwa zimekua zikichangia ongezeko la soil acidity Ikitumika katika ratio ya lita moja ya Mkojo wa Sungura kwa lita 5 za maji kunyunyuzia katika majani au ardhi wakati wa asubui au jioni kipindi ambapo stomata zipo wazi itakupa matokeo mazuri katika viazi,maharage,miche ya matunda, mbogamboga, mahindi na mazao mengine
Lakini pia Kama kimiminika cha asili chenye uwezo wa kurudisha rutuba iliyopotea ardhini Matumizi ya Mkojo wa Sungura Kama kiuatirifu (insecticides) Mkojo wa Sungura una,kiasi kikubwa cha Ammonia ambayo ndio makali yake halisi ambayo Uharibu kabisa mazingira rafiki ya uzalianaji wa bacteria na fangasi katika mmea Mkojo wa Sungura ukitumika kwa kiasi cha lita 1 katika Lita 2 hadi 3 za maji kunyunyuzia katika majani ambayo yameshambuliwa na wadudu kila siku,huua wadudu na kurejesha afya ya mmea Mkojo wa Sungura huua wadudu kama aphids,fungus, mites ,leaf miners nk
Katika mmea ambao haujashambuliwa, ukinyunyuzia kwa wiki Mara,moja inatosha kuupatia mmea afya bora,ustahimilivu wa magonjwa ya bacteria na fangasi pia kukupatia mavuno mengi
Mbolea ya mkojo wa sungura ni mbolea bora zaidi yenye kuleta faida kubwa kwenye udongo kwani ina uwezo wa kufufua ardhi iliyokufa ambayo ilikua haifai kwa matumizi ya kilimo pia huleta faida kwa mkulima kwa kuongeza kipato kwa ongezeko la uzalishaji shambani kwake.
Mbolea hii ina virutubisho vingi ndani yake ikiwemo nitrogen, phosphorus, pottasium na virutubisho vingine vidogo vidogo ( micro nutrients) kama vile calcium, magnesium, boron, zinc, manganese, sulfur,copper, cobart na vingine vingi ikiwemo na wadudu wadogo wadogo wanaohitajika katika udongo ( micro organisim)
Angalizo;-
Usitumie Mkojo wa Sungura ambao haujachanganywa na maji.
Ni Habari mpya ni vema kuendelea kufanya uchunguzi - Chimala Mkoani Mbeya mkojo wa Sungura unatumika sana mashambanikama mbolea na viwatilifu pia
JibuFutaNi kweli kabisa
FutaSungura hamsini kwa wiki moja wanauwezo wa kutoa lita ngapi za mkojo?
JibuFutahabari ya jioni
JibuFutaNaomba kuuliza mkojo WA sungura soko lake ni wapi kwa mkoa WA Arusha na bei pia kwa kwenye idea
habari ya jioni
JibuFutaNaomba kuuliza mkojo WA sungura soko lake ni wapi kwa mkoa WA Arusha na bei pia kwa kwenye idea