MAGONJWA YANAYOSUMBUA ZAO LA MUHOGO SHAMBANI
Zao la mhogo halina magonjwa mengi lakini ugonjwa wa "Cassava
Mosaic" na Batobato ndiyo yanayoathiri sana uzalishaji wa zao hili.Ugonjwa huu
husababishwa na virusi na huenezwa na nziwadogo weupe.Mmea ulioathirika
ukitumika kwa vipando mche mpya nao utakuwa na ugonjwa huu.Majani ya mmea
ulioshambuliwa yatakuwa na rangi ya njano na yasiyo na umbo la kawaida.
Kuzuia ugonjwa huu-panda aina ya muhogo inayostahimili ugonjwa
huu,Panda vipandikizi ambavyo havijatoka katika mmea ulioathirika na ugonjwa
huu,pia unaweza kuchovya mbegu ulizokata katika maji ya moto kwa muda mfupi na
kwa tahadhari kubwa.Pia tumia dawa za wadudu kuua nzi weupe.
Kuna magonjwa mawili ambayo yanasababisha kupunguza uzalishaji wa
zao la muhogo shambani.
(A)UGONJWA WA MATEKENYA/ MICHIRIZI YA KAHAWA KATIKA
MUHOGO.
Huu ni ugonjwa ambao unapatika katika sehemu za miinuko iliyo na
urefu chini ya mita 300 na unapatika katika sehemu ndgo katika maeneo ya miinuko
ya mita 500.Ugonjwa huu unaenezwa na mdudu mweupe au inzi mweupe (whitefly)
mwenye mabawa madogo.
Dalili za ugonjwa kwenye mmea wa muhogo.
Hapa tutaangalia katika sehemu tatu za mmea wa muhogo
(I)KATIKA MAJANI
Dalili ya kwanza:hutokea rangi ya njano pembezoni mwa vena ndogo
baadae huathiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa la rangi ya njano.
Dalili ya pili:rangi ya njano ambayo haihisishwi vizuri na vena
isipokuwa katika mabaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za
ugonjwa sehemu kubwa lamin inaweza isiathirike,majani yenye ugonjwa hubaki
yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.
(II)KWENYE SHINA
Ugonjwa huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani lakini jeraha
la zambarau au kahawia linawweza kuonekana nje na kuingia ndani hadi kwenye
gamba baada ya kubandua gome la nje.
(III)KWENYE MIZIZI
Kifo cha mzizi hutokea kuanzia miezi mitano toka kupandwa,dalili za
mizizi huonekana kubadili nje ya mizizi na zinaweza kuwa kama kizuizi mwanga au
shimo au kufa kwenye gome.Tishu inayozunguka mashina ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi,wakati mwingine mizizi huonenekana kuwa yenye afya kwa nje
bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa,lakini ikikatwa
huonekana kufa.Ugonjwa huu uenezwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye
mimema iliyoathiriwa.
(B)UGONJWA WA BATOBATO/UKOMA WA MAJANI
Ugonjwa huu ulienea Tanzania kataka miaka ya 1894 na kuripotiwa
katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.Ugonjwa huu usababishwa na inzi mweupe
lakini uchunguzi wa mara kwa mara umetambua kuwepo kwa virusi vya aina
mbalimbali kama vile; Afrika cassava mosaic virus na Indian cassava masaic virus.
Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
-Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.Piakloritiki ya
jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe yenye
kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.
Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri
sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za awali za
ukuaji wa jani.
Pia majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja
na kujitenga kwa sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
Ugonjwa huu huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa
kawaida hutumika kuzalishia mmea.
JINSI YA KUDHIBITI MAGONJWA HAYA SHAMBANI MWAKA
-Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya
mihogo unatakiwa kuchoma moto ili kutokomeza ugonjwa huo
-Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa
kung’oa ile Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
-Pia unahitajika kuelewa dalili za magonjwa kwa ajili ya kuchukua
tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni