KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI
KILIMO BORA CHA PILIPILI MBUZI : Pilipili mbuzi ni zao ambalo
linaweza kulimwa kibiashara na kumpatia faida nzuri mkulima. Zao
hili huitaji mwanga wa kutosha wa jua angalau kiasi cha masaa 6
kwa siku.
Pilipili hustawi vizuri zaidi kwenye udongo wenye mbolea ya asili,
undongo wenye unyevu nyevu ila usiwe wenye kutuamisha maji.
Pilipili mbuzi huitaji udongo wenye pH 6.0 hadi 6.8, Ikiwa pH ni chini
ya 6.0 ongezea madini chokaa kwenye udongo; Na ikiwa pH ya
udongo imefika 8 onana na wataalam wa kilimo wakusahuri namna
ya kuipunguza.
Kuandaa miche.
Mbegu za pilipili huoteshwa miche kwenye kitalu kabla ya kwenda
kupandikizwa shambani. Pandikiza mbegu kwenye kitalu week 7 hadi
10 kabla ya kipindi ambacho umepanga kupandikiza miche
shambani. Panda mbegu tatu tatu kwenye kila kishimo na chagua
mbili zilizo chipua vizuri kwa ajili ya kuhamishia shambani.
Kuhamishia miche shambani.
Hamisha miche shambani ikiwa imetengeneza majani 8, ingawa
kuhamisha ikiwa na majani machache au mengi zaidi haitapelekea
shida yoyote.
MUHIMU… Unashauriwa kuhamisha miche shambani kwa kuzingatia
mambo yafuatayo.
Siku ya kwanza kwa lisaa limoja weka miche kivulini au mahali
ambapo kuna kizuizi jua la moja kwa moja lisiifikie miche. Kadri
siku zinavyo kwenda ruhusu miche kupata mwanga wa jua zaidi.
Chimba mashimo marefu kuzidi urefu wa mizizi ya miche kisha
changanya vyema udongo na mbolea ya Ngo’ombe. Muda mzuri
wa kuhamisha miche yako shambani ni jioni au kipindi ambacho
jua limefifia kuepuka miche kukauka.
Changanya sulphur (Tembe 2) kwenye maji na kumwagilia na
rudia mchanganyo huu kila baada ya week mbili. Sulphur husaidia
kuuwa fungus, inauwa bacteria wasio faa, kuzuia magonjwa pia
huasaidi mizizi kusambaa na kukua kwa haraka na kupata
virutubisho.
Mwagilia miche maji ya kutosha baada ya kuihamishia shambani
hiyo husaidia kupunguza stress za mmea unapobadilishiwa
mazingira. Tumia mbolea ya Miracle Gro kila baada ya week mbili.
Mahitaji ya mmea.
Pilipili ni zao lenye kuhitaji zaidi unyevu unyevu shambani ila maji
yasiwe yenye ktuama. Kipindi ambacho maua yametoka na vitunda
vya pilipili vimeanza kujitokeza, udongo ukiwa mkavu sana hauna
unyevu wa kutosha hupelekea maua kudondoka. Epuka umwagiliaji
ulio zidi mahitaji au ulio chini ya mahitaji. Unaweza kutandaza nyasi
kwaajili ya kusaidia kuhifadhi unyevu shambani. Mmea huanza kutoa
maua mapema baada ya kutengeneza matawi, Maua ya mmea hua
na set iliyo kamilika (jike na dume) hivyo kuwa na sifa ya kuweza
kujichavusha yenyewe.
Upepo, wadudu au kwakutumia mkono husaidia kuongeza
uchavushaji.
MBOLEA
Siku 10 Baada ya kupanda sasa endelea kukuzia mbolea,wakati huu
tumia Yaramila winner 5-10g kwa mche.NB:Usitupie juu..hakikisha
mbolea unaifukia kuzunguka mmea na usiweke karibu sana na
mmea,weka 4-6 cm kutoka kwenye mmea.
Na kila baada ya siku 21 weka mbolea aina ya Yaramila winner au
NPK Isipokuwa wakati maua yameanza weka Yaramila nitrabo au
CAN 10g /plant,na baada ya hapo utaendelea na Y-winner mpaka
mwisho wa mavuno.
KUPALILIA
Pilipili zi zao ambalo halina mizizi merefu sana, hivyo basi mkulima
anapaswa kuzingatia hilo na kuongeza umakini wakati wa kupalilia
kuepuka kukata mizizi.
MAGONJWA
1. Fusarium wilt (Mnyauko)
Njinsi ya kuepuka. .Tandika shamba lako na majani makavu ili
kupunguza joto.
Ng’oa mimea yote iliyougua na choma moto mabaki.
Epuka kusambaza ugonjwa kwa kusafisha vizur vifaa vya shamba
na chini ya miguu uingiapo shambani.
Jitahidi mimea iwe na afya nzuri kwa kuweka mbolea na maji ya
kutosha.
Pulizia dawa ya fangas kama vile ortiva.
2) Southern blight ( Sclerotium wilt)
Huu ungonjwa utaona kwenye shina china panaota fangasi
weupeweupe (Whitish fungal growth on the stems of infected
plant) .Majani ya chini huweza kunyauka,Huu ungonjwa hutokea
muda mfupi kipindi cha joto kali.
Kuepuka/Kuzuia.
Wakati wa kulima ..lima hadi chini sana ili hao fangasi waende
chini sana ambapo mizizi haifiki.
Mimea iliyoshambuliwa…Ing’oe yote na choma moto lakini chomea
nje ya eneo la shamba.
Pulizia Ortiva.
3) Anthracnose.
Huu ni ugonjwa wa kawaida kwenye pilipili mbuzi na huu ugonjwa
huweza kukaa ardhini muda mrefu.Dalili zake utaona matunda kama
kuna sehemu zinakuwa nyeusi na panajaa majimaji …dalili hii huenea
sehemu kubwa ya tunda na baadaye tunda huoza.
Kuepuka.
Kuepuka ugonjwa kujirudia musimu na musimu..Baada ya kuvuna
choma mabaki yote.
Shamba ambalo ulilima pilipili usirudie kulima pilipili mfululizo
zaidi ya mara mbili…badilisha zao kwa kupanda zao ambalo sio
jamii moja na pilipili mbuzi (Do crop rotation).
Pia huu ugonjwa huweza kupitia mbegu…kwa hiyo mkulima lazima
achukue mbegu kutoka kwa wakala aliyeidhinishwa na
mwaminifu…mbegu hazitakiwi kutengenezwa kutoka kwenye
mimea iliyoathirika na ugonjwa.
4) Bacteria.
Madoamadoa ya bacteria kwenye matunda….huweza kutokea na
kusambaa haraka wakati wa joto kali na unyevu kwenye udongo.Pia
huu ugonjwa huweza kuenea kupitia mbegu.
Dalili zake utaona madoamadoa ya kama brown chini ya majini na
pia kwenye matunda.
Kuepuka.
Usitengeneze mbegu kutoka kwa mimea iliyoathirika na huu
ugonjwa.Nunua kutoka kwa wakala.
Pulizia dawa yoyote copper.
5) Virusi.
Kuna aina nyingi ya virusi ambao hushambulia pilipili mbuzi.
Dalili zake ni majani kuwe ba njano na kujikunja .
Kuepuka.
Nunua mbegu bora
Pulizia dawa za wadudu kuanzia kwenye kitaru na
kuendelea.Wadudu wanaosababisha virus sanasana na wadudu
mafuta (Aphids) kwa hiyo akikisha muda wote shambani hakuna
hao wadudu kwa kupulizia Actara.
NB:Pamoja na maelezo yote hapo juu.Usikae zaid ya siku 14 bila
kupiga dawa ya wadudu na ukungu/fangasi hata kama hakuna
ugonjwa.
Wadudu.
Pilipili mbuzi hushambuliwa na ;
1. Wadudu mafuta ( Aphids)
Kuwadhibiti.
Tumia Actara 8g/20L.
Au tumia wadudu wanaokula wadudu mafuta,mfano special beetles.
2. Crickets
Hawa wadudu hukaa aridhini karibu na mmea na usiku hutoka
walipo jificha na kukata miche michanga.
Kawadhibiti.
Unapo andaa shamba andaa vizur ili nyumba zao zife na kuwaacha
katka halu ya hatari ya kuliwa na ndege na wadudu wengine ,kama
ni miche na iko kwenye tray…basi weka hizo tray juu ya kichanja.
3. Beetle.
Tuma Karate 40cm/20L.
4. Utitiri
Dawa:Tumia Dynamec au yoyote yenye Abamectin.
5. Nematodes
Tumia solvigo.
Mavuno.
Pilipili huwa tayari kwa kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemea na aina
ya mbegu uliyotumia. Chuma kwa uangalifu bila kung’oa mmea ili
uendelee kuzalisha. Muvuno yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi
1 hadi 3.
Usalama wakati wa uvunaji.
Pilipili huwa na kemikali iitwayo capsaicinoids ambayo inaweza
kukuwasha kwenye ngozi au kwenye macho ikiwa utajigusa. Vaa
gloves wakati wa kuvuna na kuwa mwangalifu usijiguse kwenye
macho.
SOKO
Fursa
Pilipili ni zao ambalo halina mbadala wake au (substitute) hivyo
kufanya mahitaji yake kuwa ni ya muda wote bila kutetereka.
Changamoto
Muda ambao wakulima wengi wanakuwa wamezizalisha zaidi
huathiri sana soko la pilipili kwa maana hata bei ikishushwa sana
haiwezi kushawishi watumiaji kutumia pilipili nyingi zaidi.
Kuepuka changamoto hiyo wakulima wanashauriwa kupunguza
huduma shambani hadi pale soko litakapo tengemaa vizuri.
Mbinu za mafanikio kwenye kilimo hiki.
1. ZALISHA KWA WINGI
Uzalishaji mkubwa husaidia sana kupunguza gharama ambazo
haziepukiki yani (Fixed Cost). Ukizalisha kwa wingi kwa gharama
ndogo utaweza pia uza bidhaa zako kwa bei ndogo na bado utapata
faida nzuri na kujihakikishia soko la uhakika kwa bidhaa zako.
2. TAFUTA MASOKO YA BIDHAA KABLA YA KUANZA UZALISHAJI
Mkulima mwenye mafanikio ni lazima pia awe mfanya biashara mzuri
ukiachilia mbali kuwa mzalishaji mzuri. Mkulima ni vyema
kutengeneza channels mapema kupata wateja wa mazao yako.
Ukizalisha kwa wingi kwa gharama ndogo itakusaidia sana kwenye
kupata masoko utakwa na ushawishi zaidi kwa wateja. Tengeneza
wateja na wateja watakutengenezea biashara.
Mteja anataka vitu vitatu vya msingi.
Unafuu wa bei
Ubora wa zao
Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa
Ukijihakikishia hivyo vitu vitatu hapo juu hapana shaka utakuwa
umejihakikishia soko la uhakika.
3. USILIME KWA KUFUATA MSIMU
Unapolima kwa kufuata msimu, mtajikuta wakulima wengi
mmezalisha zao fulani kwa wiiingi kwa kipindi kimoja hivyo kupelekea
upatikanaji wa zao hilo kuwa mkubwa kuliko inavyo hitajika kwenye
masoko, jambo hili hupelekea mazao kuuzwa kwa bei ndogo na
kupelekea wakulima kukosa faida ya kutosha au hata kupata hasara
muda mwingine.
Unapolima kwa kutofata msimu mkulima utaweza kuazalisha zao/
mazao kipindi ambacho wengine hawazalishi hivyo mahitaji
yatakuwa makubwa na upatikanaji wa zao hilo utakuwa ni mdogo
hivyo mkulima ataweza kupanga bei nzuri kwa mazao yake.
4. USIFANYE KILIMO KWA MAZOEA
Tumia wataalamu wa kilimo
Tumia njia za kisasa za kilimo
Fanya utafiti wa ardhi dhidi ya zao unalotaka kufanya (Tumia
wataalamu)
Fanya kilimo cha umwagiliaji uweze kuzalisha kipindi ambacho
wengine hawawezi kuzalisha ili uuze mazao yako kwa bei nzuri
zaidi,
FAIDA ZA KUTUMIA PILIPILI
1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu.
2. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene
(overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa
mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti
iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi
Julai 2006.
3. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili
kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha
insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.
4. Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na
vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata
nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu
moja ya mwili.
5. Pilipili husaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba
kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi.
6. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye
tumbo (Stomach Cancer).
7. Pilipili husaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo
husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua
kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.
8. Kula pilipili husaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi
cha fibrin katika damu
Jumapili, 28 Januari 2018
Kilimo cha pilipili mbuzi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA
JIFUNZE KUFUGA KIBIASHARA HASA KWA WAFUGAJI WA KUKU KWA YOYOTE ATAKAYE HITAJI TEMPLATE HII NA ZINGINE ANITAFUTE KWENYE NO 0756841313

-
MAAJABU YA MKOJO WA SUNGURA Licha ya kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kwaajili ya nyama, zao la Mkojo wa Sungura kwa faida yake pengin...
-
Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu. Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi k...
-
UTANGULIZI koroshoo ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae 16 century ndipo lilipo fika africa katika nchi ya mozamboque na b...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni