Jumanne, 20 Februari 2018

Kuku kutokutaga

SABABU ZA KUKU KUTOTAGA
Kuku hupunguza utagaji na hata kuacha kutaga kabisa iwapo:-
 Hawakupewa chakula bora au cha kutosha.
 Hawapewi maji safi ya kutosha.
 Wamebanana, yaan hawakai kwa raha.
 Vyombo vya maji au chakula havitoshi.
 Mwanga hautoshi.
 Majogoo yamezidi (weka jogoo 1 kwa mitetea 10)
 Kuku wanaumwa.
 Wana vidusa vya nje na ndani (external and internal parasite).
 Wamezeeka (umri zaidi ya miaka miwili na nusu).
 Maumbile ya kuku mwenyewe.

NINI KIFANYIKE
 Wape kuku chakula bora na cha kutosha (gram 110 - 120 kwa kuku kwa siku).
 Wape maji safi ya kutosha, wanywe maji saa moja zaidi baada ya kuwalisha
chakula.
  Weka idadi ya kuku inayolingana na nafasi iliyopo. Weka kuku 3 - 4 kwa
meta moja mraba.
 Weka vyombo visafi na vya kutosha.
 Hakikisha chumba kina mwanga wa kutosha. Mwanga unaowatosha kuku ni
ule unaoruhusu mtu kusoma gazeti.
 Weka idadi ya vyombo kulingana na mitetea iliyopo. Jogoo 1 kwa mitetea 7 -
10.
 Watenge na kutibu kuku wagonjwa. Na wachanje kuku ukifuata kalenda.
 Tibu vidusa vya ndani na nje (external and internal parasite) kwa kufuata
ratiba au kila unapoona dalili.
 Ondoa kuku wazee kwa kuuza au kuchinja.
 Ondoa kuku wasio taga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA

JIFUNZE KUFUGA KIBIASHARA HASA KWA WAFUGAJI WA KUKU KWA YOYOTE ATAKAYE HITAJI TEMPLATE HII NA ZINGINE ANITAFUTE KWENYE NO 0756841313