Jumapili, 28 Januari 2018

Kilimo cha hydroponic fodder kwa kutumia plastiki ya dumu

UTANGULIZI
HYDROPONIC ni sayansi/sanaa ya
kuotesha mazao bora yenye tija kwa
muda mfupi zaidi bila kutumia
udongo kabisa, kwa kutumia maji na
virutubisho (Hydroponic Nutrients).
HYDROPONIC HYDROPONICS FODDER
– ni kimea kinachooteshwa kwa
kutumia mbegu za shayiri au ngano
ili kupata chakula cha mifugo mfano
kuku, ng’ombe, sungura, nguruwe,
mbuzi, kondoo n.k
Ili kuotesha mbegu zako kwa utaratibu
huu utahitaji kuwa na banda maalum
kwa kuoteshea lenye ukubwa wowote,dumu la rita ishirini la maji Pia utahitaji kuwa na virutubisho vya
hydroponics (Hydroponics Nutrients),
Sprayer (Chupa ya kunyunyiza maji
yenye matundu madogo ili maji
yamwagike kama mvua), Mbegu za
shayiri au ngano (chagua mbegu
ambazo hazijashambuliwa na
wadudu), na pia unatakiwa uwe na
chombo cha kuloweka mbegu na hapa
waweza kutumia ndoo ya aina yoyote,
kwani itatakiwa uziloweke kwa siku
chache.
Sayansi hii ya uoteshaji wa mbegu
mbalimbali madhumuni makubwa
sana ni kwaajili ya mifugo kama vile,
Kuku, Mbuzi, Ng’ombe, kondoo na
kazalika, ila kama ni mboga inaweza
itwa hydrponic tomatoes na kazalika
kulingana na aina ya mbegu husika.
FAIDA YA MATUMIZI YA HYDROPONIC
Ili kuweza kukupatia picha halisi
tunakufahamisha kwanza faida
zilizopo za matumizi ya hydroponic
fodder kwa mifugo.Kwa uchache
baadhi ya faida hizo ni:
• Ni nafuu sana kulinganisha na
garama za CHAKULA cha madukani au
viwandani.
• Kina virutubisho na vitamini mara
3 zaidi ya CHAKULA cha kawaida cha
Mifugo.
• Hupunguza magonjwa ya mfumo
wa hewa kama vile mafua kwa
mfugaji na Mifugo kwani hakina
vumbi kabisa.
• Kina protein na Energy/nishati
nyingi zaidi mara 3 ya inayopatikana
kwenye vyakula vya kawaida vya
Mifugo kama kuku.
• Mifugo hukua haraka sana
kutokana na wingi wa protein ambayo
hufanya Kazi ya kujenga mwili na
kukuza.
• Chakula hiki ni laini sana na
kitamu kwa kuku na mifugo yote
(palatable).
• Mmeng’enyo wa chakula hiki
huongezeka kutoka 30% kwa chakula
cha kawaida hadi 95% kwa chakula
cha hydroponiki hivyo chakula kingi
kutumiwa na mwili wa mifugo na
kupunguza kinyesi na usumbufu wa
usafishaji wa banda.
• Kinyesi hupungua na kuwa kati ya
5%-10% tu kwani chakula kingi
humeng’enywa na kutumiwa na mwili
wa mifugo.
• Mazao kama mayai au maziwa
huongezeka kwa 40% kulinganisha na
chakula cha kawaida.
• Kiini cha yai la kuku anayelishwa
hydroponic fodder huwa cha njano
sana hata kama ni kuku wa kisasa.
• Hupunguza garama za ufugaji
kwenye manunuzi ya chakula kwa
50-75% hivyo kuongeza faida.
Pamoja na mnyumbulisho wa baadhi
za faida ya matumizi ya teknolojia hii
hapo juu,kiujumla ni rahisi kutumia
teknolojia hii kwani inaweza
kufanyika mahali popote. Husaidia
kuvuna na kupata mazao mengi kwa
muda mfupi. Haina madhara kwa
afya za mifugo na binadamu kama
mlimaji alizingatia maelekezo.
JINSI YA KUANDAA
Tumefanya tafiti kufahamu hatua
kadhaa zinazopitiwa ili kufanikisha
zoezi la upandaji.Zifuatazo ni baadhi
ya hatua ambazo tumefanikiwa
kukutana nazo:
• Chukua mbegu zako kisha zisafishe
vizuri kuondoa takataka zote.
• Weka maji kwenye ndoo safi na
kisha weka mbegu zako ili kuziloweka
kwa muda wa masaa 4 au zaidi
ukipenda masaa 12.Muda mrefu zaidi
huwezesha mbegu kuchipua vizuri na
kwa haraka.
• Baada ya masaa 4 au 12 kupita toa
mbegu zako kwenye ndoo na uzichuje
maji kwa kutumia chujio au kitambaa
kisafi.
• Baada ya kuchuja maji hamishia
mbegu zako kwenye dumu ulilolikata katika pande mbili kama inavyoonyesha kwenye picha kisha
zisambaze ili zisibanane kupita kiasi.
Kwa kuanzia fursa hii unaweza
kutumia tray yeyote hata ungo unafaa
kwa kuanzia .

• Baada ya kuweka mbegu zako
funika dumu yako kwa
muda wa masaa 48 (SIKU 2) tumia
mfuniko wenye matundu madogo
madogo na machache.
• Baada ya masaa 48 kupita (siku 2)
mbegu zako zitakuwa zimechipua
kikamilifu, utaona mfano wa nyuzi
nyeupe zinachomozo.
• Hamishia dumu zako kwenye
kichanja au eneo lenye hewa ya
kutosha lakini zikinge dhidi ya jua
kali kwa kuweka turubai au nailoni
juu ya kichanja unaweza pia kutumia
hata mifuko ya unga (viloba)
kutengeneza kichanja, unaweza pia
kuzungusha wavu kama net za mbu ili
kuzuia wadudu i.e inzi na pia kama
eneo lako lina ndege wengi basi
kutumia net itakuwa msaada kwako ili
kuwazuia ndege hao.
UMWAGILIAJI
Mwagilia angalau mara 3 kwa siku,
yaani asubuhi, mchana na jioni.
Hakuna haja ya kumwagilia usiku kwa
sababu hewa ya usiku huwa imepoa
na kubeba unyevu wa kutosha na hata
asubuhi usishangae kukuta umande
kwenye fodder yako.
UVUNAJI
Unaweza kuvuna fodder yako ndani
ya siku 7 au 9.Ingawa wapo wengi
wanavuna haraka yamkini ili kukidhi
uhitaji kwa wakati husika.Lakini
makala nyingi zinaelekeza siku 7 au
9.

Maoni 2 :

  1. Kwani zaidi Ngano au shayiri hakuna mbegu zingine za kuotesha hydroponic

    JibuFuta
    Majibu
    1. zipo mbegu nyingine nyingi hata mboga unaweza panda kwa kutumia kilimo hiki

      Futa

UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA

JIFUNZE KUFUGA KIBIASHARA HASA KWA WAFUGAJI WA KUKU KWA YOYOTE ATAKAYE HITAJI TEMPLATE HII NA ZINGINE ANITAFUTE KWENYE NO 0756841313