Kilimo cha hydroponic nikilimo ambacho hakitumii udongo katika ukuzaji wa mazao teknolojia hii hutumika katika ukuzaji wa mazao ya bustani pia hutumika kukuza chakula cha wanyama kijulikanacho kama hydroponic fodder
Kwa nini Kilimo hiki hakiitaji udongo kwasababu kazi ya udongo kwenye mmea ni kuupa mmea virutubisho ili uweze kukua katika Kilimo hiki virutubisho hupatikana katika maji ambayo yamechanganywa Na virutubisho ivyo Na kusambazwa kwenye mimea Na mmea utapata virutubisho kama ipatavyo kwenye udongo
Kilimo hichi kinamifumo mbalimbali ya usambazaji wa hizo nutrient baadhi ya mifumo hiyo ni
Kusambaza kwa kutumia drip irrigation njia hii ni njia ambayo hutumia vifaa vya drip irrigation lakini mazao yako yanatikiwa yawe yamepandwa kwenye makopo katika makopo hayo hautatumia udongo Bali unaweza ukatumia makutu ya minazi au mabaki ya pamba ili kuusimamisha mmea wako
Pia unaweza ukasambaza virutubisho kwa kupanda mazao yako kwenye mabomba ambayo yapo kama mabomba ya maji yalio tobolewa kwaajili ya kuweka mazao yako ambapo katika mfumo huu maji yenye virutubisho yatakuwa yanapita ndani ya bomba kwa ratiba au kwa mda maalumu maana yake maji ayo yatapita kwa muda kama ni kila baada ya lisaa limoja itabidi kuyapitisha maji hayo yenye virutubisho ndani ya bomba
Pia unaweza kupanda kwenye makontena ambapo utatumia kontena ambalo linamfuniko Na lina tunza maji halivujishi utafanyaje unatakiwa kutumia vikopo ambavyo vitakuwa vimetobolewa chini matundu madogo ambayo yanapitisha maji kisha utajaza mabaki ya pamba au makuti ya minazi Na kuweka mimea yako kisha utatoboa mfuniko wa kontena matundu ambayo kikopo chako ulichopanda mmea kitaingia alafu unaweka maji kwenye kontena kufikia kimo ambacho kikopo kitakuwa kinaingia kwenye maji angalau nusu Na kufunika konten Na kuweka vikopo kwenye matundu uliotoboa kwenye kontena
Kunamifumo mingi lakini ninaifahamu hiyo michache
Katika Kilimo hiki Miche hukuzwa kwenye trey za kukuzia Miche ambapo hautatumia udongo ila utatumia mabaki ya pamba au makuti ya minazi kukuzia lakini utakuwa unamwagilia maji yenye virutubisho
Kwenye hydroponic fodder yaani chakula cha wanyama mbegu za shayiri hutumika ambapo hupandwa kwenye trey za aluminiam Na huweki kitu chochote zaidi ya mbegu Na kumwagilia maji yenye virutubisho mpaka zitakapo fikia mda wa kuvuna
Faida za Kilimo hini ni Kilimo ambacho hakiitaji upaliliaji pia kina zuia magonjwa yatokanayo Na udongo, hakichagui msimu wa kulima unalima mda wowote pia kinakupa mazao yaliyo bola Na faida nyingine nyingi
Jumapili, 15 Oktoba 2017
kilimo cha hydroponic
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA
JIFUNZE KUFUGA KIBIASHARA HASA KWA WAFUGAJI WA KUKU KWA YOYOTE ATAKAYE HITAJI TEMPLATE HII NA ZINGINE ANITAFUTE KWENYE NO 0756841313

-
MAAJABU YA MKOJO WA SUNGURA Licha ya kuwa wafugaji wengi wamekuwa wakifuga kwaajili ya nyama, zao la Mkojo wa Sungura kwa faida yake pengin...
-
Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu. Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi k...
-
UTANGULIZI koroshoo ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae 16 century ndipo lilipo fika africa katika nchi ya mozamboque na b...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni