Jumatatu, 29 Oktoba 2018

Rutuba ya udongo

Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu.
Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya
kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho.
Vipengele vingine vya ukuaji kama vile mwanga, nyuzi joto na maji viko katika hali inayofaa. Uwezo huu hautegemei kwenye wingi wa virutubisho kwenye udongo peke yake, lakini pia kwenye ufanisi wa kubadilisha virutubisho ndani ya duara la virutubisho shambani.
Sifa za udongo wenye rutuba
Una virutubisho vingi muhimu kwa ajili ya lishe ya msingi ya mmea (ikiwemo naitrojeni,
fosfora, potashiamu, kalishamu, magnesia na salfa).
Una virutubisho vya kutosha vinavyohitajika kwa kiwango kidogo sana na mmea (ikiwemo boroni, kopa, chuma, zinki, manganizi, klorini na molibdenam).
Una kiasi stahiki cha mabaki ya viumbe hai kwenye udongo.
Una kipimo cha pH katika kiwango kinachofaa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao (kati ya 6.0 na 6.8).
Una muundo unaomeng’enyuka.
Uko hai kibiolojia.
Una uwezo mzuri wa kuhodhi maji na kutoa virutubisho.
Kiasi stahiki cha virutubisho vya mmea
Kuna aina 16 ya virutubisho muhimu ambavyo mimea huhitaji ili kukua vizuri. Kati ya elementi hizi 16 muhimu; haidrojeni, kaboni na oksijeni hupatikana kwa sehemu kubwa kutoka kwenye hewa na kwenye maji.
Elementi nyingine muhimu hutoka ardhini na kwa ujumla, husimamiwa na wakulima. Baadhi ya virutubisho hivi huhitajika kwa wingi katika tishu za mmea na huitwa ‘virutubisho vikubwa’.
Virutubisho vingine vinahitajika kwa kiasi kidogo hivyo huitwa ‘virutubisho vidogo’. Virutubisho vikubwa vinajumuisha naitrojeni (N), fosfora (P) potashiamu (K), kalishamu (Ca), magnezia (Mg) na salfa (S).
Kati ya hizi N, P na K kwa kawaida huisha ardhini kwanza kwa sababu mimea inayahitaji kwa wingi kwa ajili ya ukuaji na maendeleo yake, hivyo hujulikana kama virutubisho vya msingi.
Ni nadra kwa Ca, Mg na S kuwa kikwazo kwa ukuaji wa mmea, hivyo hujulikana kama virutubisho vya umuhimu wa pili. Pale ambapo udongo una asidi, chokaa mara nyingi huongezewa, ambayo ina kiasi kikubwa cha kalishamu na magnezia.
Salfa kwa kawaida hupatikana katika mabaki yanayooza ya viumbe hai. Virutubisho vidogo ni: boroni (B), kopa (Cu), chuma (Fe), kloraidi (Cl), manganizi (Mn), molibdenam (Mo) na zinki (Zn).
Kurejeshea mabaki ya viumbe hai kama vile mabaki ya mazao na majani ya miti ni njia bora ya kuipatia mimea inayokua virutubisho vidogo.

UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA

JIFUNZE KUFUGA KIBIASHARA HASA KWA WAFUGAJI WA KUKU KWA YOYOTE ATAKAYE HITAJI TEMPLATE HII NA ZINGINE ANITAFUTE KWENYE NO 0756841313